Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ishu ya Daka mashabiki watolewa hofu

Muktasari:

  • Ripoti katika mitandao ya kijamii zilidai, mshambuliaji huyo wa Leicester City aliteleza wakati wa kusherehekea bao hilo, hali iliyozua hofu kuwa huenda alipata jeraha.

DAKTARI wa timu ya taifa ya Zambia, Wesley Ngongo, amewatoa hofu mashabiki na kutaka kuzipuuzia mbali tetesi zilizosambaa mitandaoni kuwa mshambuliaji Patson Daka alipata jeraha la shingo wakati alipoanguka akisherehekea bao lake kwa mtindo wa kuruka samasoti.

Ripoti katika mitandao ya kijamii zilidai, mshambuliaji huyo wa Leicester City aliteleza wakati wa kusherehekea bao hilo, hali iliyozua hofu kuwa huenda alipata jeraha.

Hata hivyo, Dk. Ngongo amekanusha hofu hizo na kuthibitisha kuwa Daka yuko fiti na hana maumivu yoyote.

“Ningependa kuwahawakikishia wote kuwa, Patson yuko sawa kwa asilimia 100. Hana jeraha lolote. Ni kweli soka ni mchezo wa kugusana; wachezaji hukimbia, wakati mwingine hujikwaa au huanguka, lakini hawawezi kuumia kutokana na miguso midogo au kuanguka kwa kawaida,” alisema Dk. Ngongo.

Aliongeza, Daka aliyeisaidia Zambia kuokoa pointi dhidi ya Mali, hana maumivu yoyote, hana mkazo wa shingo wala tatizo jingine lolote.

“Hana maumivu, hana kukakamaa kwa shingo. Uwezo wake wa kuzungusha shingo uko vizuri kabisa na yupo tayari kushiriki mazoezi kikamilifu leo.”

Dk. Ngongo pia amewatuliza mashabiki kuhusu hali za majeraha ya Lameck Banda na Miguel Chaiwa, ambao walitolewa wakati wa mechi hiyo. Alisema wachezaji hao walipata maumivu madogo tu na watakuwa tayari kwa mazoezi.

Aidha, Lubambo Musonda naye ametangazwa kuwa yuko fiti kabisa.

“Kila mchezaji yupo tayari kwa mazoezi. Hatukuwa na jeraha lolote kubwa katika mechi ya jana (juzi). Kulikuwa na maumivu madogo tu kwa Lameck (Banda) aliyelazimika kutoka, Miguel pia alipata pigo dogo na Lubambo vivyo hivyo, lakini haya ni maumivu madogo tu. Wote wako tayari kushiriki kikamilifu mazoezi ya leo,” alifafanua.

Wakati huohuo, Dk. Ngongo amethibitisha kuwa beki mkongwe Stoppila Sunzu, aliyekosa mchezo wa kwanza dhidi ya Mali kutokana na kuugua, amepona na atarejea mazoezini.

“Mnakumbuka Stoppila Sunzu hakushiriki mchezo dhidi ya Mali kwa sababu ya maradhi, lakini sasa amepona na kuanzia leo atakuwa tayari kushiriki mazoezi kikamilifu.”