Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isak, Newcastle United wamefikia pabaya

ISAK Pict

Muktasari:

  • Mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden alipewa taarifa ya uamuzi wa klabu na gazeti la Telegraph likaripoti  hakufurahishwa na suala hilo hali iliyosababisha aendelee kufanya mazoezi mbali na kikosi cha kwanza.

NEWCASTLE, ENGLAND: STAA wa Newcastle, Alexander Isak inadaiwa amechukizwa sana na kitendo cha viongozi wa  timu yake  kumwambia wazi hatauzwa dirisha hili la majira ya kiangazi jambo ambalo limevunja matumaini yake ya kuhamia Liverpool.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden alipewa taarifa ya uamuzi wa klabu na gazeti la Telegraph likaripoti  hakufurahishwa na suala hilo hali iliyosababisha aendelee kufanya mazoezi mbali na kikosi cha kwanza.

Kutokana na hilo, Newcastle imemwambia Isak ikiwa hatokubali uamuzi huo hatocheza tena katika timu hiyo hata ikiwa atajiunga tena na kikosi.

Kocha Eddie Howe ameweka wazi kuna uwezekano Isak akaondoka lakini wamiliki wa Newcastle ambao ni waarabu kutoka  Saudia Arabia wameshikilia msimamo mkali staa huyo hatouzwa.

Liverpool walijulishwa Newcastle hawana nia ya kumuuza Isak licha ya kupokea  ofa ya takriban Pauni 110 milioni  wiki iliyopita na kutokana na hilo, Liverpool imeripotiwa kujiondoa katika mazungumzo kwani wanaona wanapoteza muda.

Inafahamika, hata kama Newcastle itamsajili mshambuliaji mpya, hawatabadili msimamo wao mkali kuhusu mustakabali wa Isak.

Howe amekuwa akifahamu msimamo wa uongozi na ameambiwa amalize tofauti zake na mchezaji ili arudi kikosini.

Uamuzi wa Newcastle kutomuuza Isak rasmi unadaiwa ni mbinu moja wapo ya kumbakisha kwani inaamini mchezaji huyo, 25, atakubali kuwa hawezi kulazimisha kuondoka klabuni, hivyo atarudi kikosini na kuendelea kucheza.

Vilevile kutokana  na tabia mbovu ambayo mchezaji huyo ameionyesha baada ya kutojumuika na kikosi kisha baadae kuonekana akifanya mazoezi na klabu yake ya zamani, Real Sociedad.

Hata hivyo, Howe amekiri ingawa angependa kuwa na Isak tena kwenye kikosi, hawezi kumjumuisha kutokana na mwenendo wake na kuna asilimia chache za kuwepo katika mechi ya ufunguzi ya Ligi Kuu England wiki ijayo.

“Tumekuwa na mazungumzo na kwa sasa ni wazi hatuwezi kumjumuisha katika kikosi. Sijui itachukua muda gani, lakini hiyo ndiyo hali ya sasa. Ningependa Alex acheze leo, ningependa afanye mazoezi kesho. Tunataka mchezaji awe nasi. Niweke wazi kabisa. Hakuna sehemu ya moyo wangu isiyotaka matokeo hayo, lakini siioni hali ya sasa ikibadilika na Isak akacheza dhidi ya Aston Villa,”alisema Howe.