Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isak atafutiwa mbadala, Semenyo atajwa

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Hadi sasa katika orodha ya wachezaji ambao inawafikiria ili kuziba pengo la Isak ni winga wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana, Antoine Semenyo, 25.

LIVERPOOL inaweza kubadili mwelekeo wa usajili iwapo jeraha la mshambuliaji wao wa kimataifa wa Sweden, Alexander Isak, 26, yataonekana kuwa makubwa na kumweka nje kwa muda mrefu.

Hadi sasa katika orodha ya wachezaji ambao inawafikiria ili kuziba pengo la Isak ni winga wa Bournemouth na timu ya taifa ya Ghana, Antoine Semenyo, 25.

Semenyo amekuwa na wakati mzuri katika kikosi cha Bournemouth tangu msimu uliopita. Mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2030.

Isak alipata majeraha katika mechi dhidi ya Tottenham ambayo aliingia akitokea benchi na kuwapatia majogoo hao bao moja.

Hadi kufikia jana Liverpool haikuwa imetoa taarifa rasmi juu ya maendeleo yake na ukubwa wa jeraha lake, lakini Kocha Arne Slot aliweka wazi staa huyo amepata majeraha yanayoweza kumweka nje kwa muda.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Isak aliyesajiliwa dirisha lililopita la majira ya kiangazi akitokea Newcastle, amecheza mechi 16 za michuano yote na kufunga mabao matatu.


Jorgen Strand Larsen

WEST HAM United imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa Wolves na timu ya taifa ya Norway, Jorgen Strand Larsen, dirisha la usajili la Januari.

Larsen, 25, ni miongoni mwa washambuliaji wanaofuatiliwa kwa karibu baada ya kuonyesha kiwango bora akiwa na Wolves licha ya timu yake kufanya vibaya.

Hadi sasa Wolves haijatoa msimamo wao ikiwa ipo tayari kumuuza au itaendelea kuwa naye. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2030.


David Moller Wolfe

ASTON Villa imejiunga rasmi katika mbio za kumsajili beki wa Wolves na timu ya taifa ya Norway, David Moller Wolfe, dirisha la usajili la Januari.

Wolfe, 23, anatajwa ni miongoni mwa mabeki wanaofanya vizuri katika Ligi Kuu England. Mkataba wa Wolfe unatarajiwa kumalizika mwaka 2030 na msimu uliopita alicheza mechi 12 za michuano yote na kufunga mabao mawili.


Niclas Fullkrug

AC Milan imeanza mazungumzo rasmi na West Ham United kwa ajili ya kuipata saini ya mshambuliaji wa klabu hiyo  na Ujerumani, Niclas Fullkrug mwenye umri wa miaka 32.

Fullkrug anatajwa kuwa tayari kupata changamoto mpya nje ya West Ham baada ya kudumu katika kikosi hicho kwa muda.

Staa huyu pia amechoshwa na hali ya kutopata nafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha kwanza. Milan inaamini atasaidia sana safu yao ya ushambuliaji kutokana na uzoefu wake.


Konstantinos Karetsas

CHELSEA inapanga kuwazidi kete wapinzani wao katika vita ya kumsajili kiungo wa Genk na timu ya taifa ya Ugiriki, Konstantinos Karetsas, 18.

Karetsas ambaye pia saini yake inahitajika na Arsenal na Inter Milan anataka kuondoka Genk ili kuendeleza zaidi maisha yake ya soka. Genk ipo tayari kumuuza fundi huyu lakini kwa kiasi kisichopungua Pauni 40 milioni.


Ayyoub Bouaddi

LIVERPOOL na Manchester United ni miongoni mwa vigogo kadhaa wa Ulaya wanaomfuatilia kwa karibu kiungo wa Lille na timu ya taifa ya Ufaransa, Ayyoub Bouaddi, mwenye umri wa miaka 18.

Lille inahitaji takribani Euro 30 milioni ili kumuuza Ayyoub ambaye ni miongoni mwa wachezaji wao tegemeo.

Mkataba wa Ayyoub unatarajiwa kumalizika mwaka 2029. Tangu kuanza kwa  msimu huu amecheza mechi 20 za michuano yote.


Axel Disasi

BEKI wa kati wa kimataifa wa Ufaransa, Axel Disasi, 27, anatarajiwa kuondoka Chelsea dirisha la usajili la Januari, huku klabu kadhaa tayari zikiwa kwenye mpango wa kumsajili.

Disasi amekuwa akipata wakati mgumu kupata nafasi ya kudumu Stamford Bridge, jambo linaloifanya Chelsea kufikiria kumruhusu kuondoka ili kupisha mipango mipya ya kikosi.

Mkataba wa Disasi unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Brennan Johnson

WINGA wa Tottenham Hotspur, Brennan Johnson, anawindwa na Crystal Palace inayotaka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji dirisha la usajili la Januari. Johnson, 24, alijiunga na Spurs akitokea Nottingham Forest mwaka 2023, lakini amekuwa hana nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza, jambo linalofanya klabu hiyo kufikiria kumwachia, ikiwa itapata ofa itakayoridhisha. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028.

Msimu huu amecheza mechi 20 za michuano yote lakini nyingi akiingia kutokea benchi.