Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Isak, Arsenal ni hivi

Muktasari:

  • Isak alikuwa mmoja kati ya wafungaji bora wa Ligi Kuu England akifunga mabao 21 na akizidiwa na Erling Haaland na Cole Palmer.

LONDON, ENGLAND: STAA wa Newcastle United, Alexander Isak amefunguka juu ya hatma yake na taarifa zinazodai huenda akajiunga na Arsenal dirisha hili.

Isak alikuwa mmoja kati ya wafungaji bora wa Ligi Kuu England akifunga mabao 21 na akizidiwa na Erling Haaland na Cole Palmer.

Newcastle ambayo ilimsajili fundi huyu mwaka 2022 kwa Pauni 63 milioni kutoka Real Sociedad inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 115 milioni ili kumuuza.

Arsenal ndio inaonekana kuhitaji zaidi ya fundi huyu na ipo tayari kumsajili katika dirisha hili kwa ajili ya kuboresha eneo lao la ushambuliaji.

Ilielezwa Newcastle ilikuwa ikihitaji  kumuuza ili kuendana na sheria za matumizi ya pesa lakini iliamua kuuza wachezaji wengine ambao ni Anderson na Yankuba Minteh.

Akizungumza juu ya suala la kutua Arsenal, Isak alisema kwa sasa hana mawazo ya kuondoka katika timu hiyo.

“Ninajisikia furaha kuendelea kuichezea Newcastle, na nimekuwa na maisha bora zaidi katika timu hii, ninapenda kila kitu kuhusu klabu, mashabiki na jiji, sina mawazo ya kuondoka kwa sasa, sijafanya mazungumzo na timu yoyote wala timu yoyote na wala Newcastle haijaniambia italazimika kuniuza.”

Katika dirisha la majira ya baridi mwaka 2022, Arsenal ilijaribu kutaka kumnunua Isak alipokuwa Sociedad lakini ikashindwa kufikia makubaliano na klabu hiyo ya Hispania.

Kocha wa Newcastle, Eddie Howe April mwaka huu, alisisitiza hawana nia ya kumuuza Isak, ambaye ndiye mchezaji ghali wa timu hiyo kwa sasa.

“Ni kipaji cha hali ya juu na hakuna kiongozi yeyote ndani ya Newcastle ambaye angetaka kumpoteza,” alisema Howe.