Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ikifika Januari bei ya Kane inashuka

Muktasari:

  • Staa huyo wa Bayern Munich yupo kwenye msimu wake wa pili Bundesliga baada ya kujiunga na miamba hiyo ya Ujerumani akitokea Tottenham ya England.

MUNICH, UJERUMANI: STRAIKA, Harry Kane atashusha bei yake anayouzwa iliyowekwa kwenye kipengele cha mkataba wake huko Bayern Munich itakapofika dirisha la Januari mwakani jambo litakalotoa nafasi kwa klabu za Ligi Kuu England kumrudisha staa huyo kwa gharama nafuu.

Staa huyo wa Bayern Munich yupo kwenye msimu wake wa pili Bundesliga baada ya kujiunga na miamba hiyo ya Ujerumani akitokea Tottenham ya England. Na baada ya kutua Allianz Arena mkataba wake uliwekewa kipengele kinachotaja bei anayouzwa endapo kama kutakuwa na timu itakayohitaji saini yake kabla ya mkataba wake kufika ukomo Bayern Munich. Kipengele hicho kilitaja bei ya Kane kuwa ni Euro 80 milioni.

Kane, 31, bado yupo kwenye kiwango bora kabisa cha kufunga, ambapo kwenye msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo, alifunga mabao 44.

Lakini, kwa mujibu wa gazeti la Bild, kipengele hicho kinachotaja bei ya Euro 80 milioni, kitashuka kwenye kipindi cha mwaka mmoja, hivyo Kane saini yake itanaswa kwa Euro 65 milioni tu Januari 2026.

Mkataba wa Kane Bayern utakwenda hadi Juni 2027 na hakika kwa sasa amekuwa na furaha kubwa kuichezea timu hiyo ambapo amekuwa na rekodi bora kabisa ya mechi kwa bao. Msimu huu ameweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefikisha mabao 50 kwa haraka zaidi kwenye Bundesliga na hivyo kuvunja rekodi hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na straika wa Norway, Erling Haaland, aliyoweka akiwa anakipiga Borussia Dortmund kabla ya kutua Manchester City.

Kane anaweza kushawishika kurudi England kwenda kupambana kuvunja rekodi ya mabao ya muda wote Ligi Kuu England inayoshikiliwa na Alan Shearer. Kane amefunga mabao 213 kwenye Ligi Kuu England na hivyo bado mabao 47 tu kufikia rekodi ya Shearer.