Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huyu ndiye Julian Quinones Kiboko ya Ronaldo

Muktasari:

  • Dakika ya tisa tu zilitosha kwa nyota huyo kuwapa raha maelfu ya Wamexico baada ya kutumia makosa ya safu ya ulinzi ya Afrika Kusini na kuandika historia kuwa mfungaji wa kwanza wa fainali za mwaka huu.

MSHAMBULIAJI wa Mexico, Julian Quinones ameweka rekodi baada ya kufunga bao la kwanza katika fainali za Kombe la Dunia 2026 wakati wenyeji hao wakicheza dhidi ya Afrika Kusini katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa kwenye Uwanja wa Azteca, Mexico City.

Dakika ya tisa tu zilitosha kwa nyota huyo kuwapa raha maelfu ya Wamexico baada ya kutumia makosa ya safu ya ulinzi ya Afrika Kusini na kuandika historia kuwa mfungaji wa kwanza wa fainali za mwaka huu.

Bao hilo ulikuwa ni mwendelezo wa msimu bora zaidi wa mshambuliaji huyo ambaye anacheza soka la kulipwa Saudi Arabia akiichezea  Al-Qadsiah.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alimaliza msimu wa Saudi Pro League akiwa Mfungaji Bora kwa mabao 33 katika mechi 31 za ligi, akiwapiku mastaa wakubwa kama Ivan Toney na Cristiano Ronaldo katika mbio za ufungaji.

Kwa mujibu wa takwimu za Saudi Pro League, Quinones alihusika moja kwa moja katika mabao 37 baada ya kufunga 33 na kutoa asisti nne, jambo lililomfanya kuwa mchezaji muhimu zaidi wa Al-Qadsiah.

Kiwango chake kilifikia kilele mwishoni mwa msimu alipofunga hat-trick katika mchezo wa mwisho dhidi ya Al Ittihad na kujihakikishia Kiatu cha Dhahabu kwa staili ya aina yake.

Wakati wengi walikuwa wakiwazungumzia Ronaldo, Karim Benzema au Ivan Toney, Quinones alikuwa akifanya mambo yake kimyakimya hadi kufikia kuwa mfungaji namba moja wa ligi hiyo yenye mastaa wengi duniani.

Safari yake imekuwa ya kipekee. Alizaliwa  Colombia, lakini baadaye akapata uraia wa Mexico na kuamua kuitumikia timu hiyo ya taifa, jambo ambalo sasa limeonekana kuwa uamuzi sahihi kutokana na nafasi yake kubwa ndani ya kikosi cha kocha Javier Aguirre.

Kwa upande wa timu ya taifa, Quinones tayari ameichezea Mexico mechi zaidi ya 20 na amekuwa sehemu ya kizazi kinachotarajiwa kuirejesha nchi hiyo kwenye mafanikio makubwa ya Kombe la Dunia. 

Miezi michache kabla ya Kombe la Dunia, Quinones pia alikuwa miongoni mwa nyota walioiongoza Mexico kuifunga Serbia mabao 5-1 katika mchezo wa kirafiki ulioonyesha jinsi safu yao ya ushambuliaji ilivyo tayari kwa mashindano hayo.