Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hugo Ekitike awapa faraja Liverpool

HUGO Pict

Muktasari:

  • Ekitike alipata jeraha baya na kupasuka kwa tendon ya Achilles ya mguu wa kulia wakati Liverpool ilipoondolewa na Paris Saint-Germain (PSG), kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Aprili 14.

LONDON, ENGLAND: MASHABIKI wa Liverpool wamepata taarifa ya kutia moyo kuhusu maendeleo ya mshambuliaji Hugo Ekitike baada ya nyota huyo kuonekana hadharani katika michuano ya Wimbledon akiendelea na safari ya kupona majeraha.

Ekitike alipata jeraha baya na kupasuka kwa tendon ya Achilles ya mguu wa kulia wakati Liverpool ilipoondolewa na Paris Saint-Germain (PSG), kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Aprili 14.

Jeraha hilo lilimlazimu kumaliza msimu mapema na pia kumkosesha nafasi ya kuiwakilisha Ufaransa kwenye Kombe la Dunia 2026. Les Bleus tayari wamefuzu nusu fainali baada ya kuichapa Morocco mabao 2-0.

Kabla ya kuanza kwa mashindano hayo, mashabiki wa Ufaransa walimpa moyo mshambuliaji huyo kwa kubeba bango lililoandikwa "Courage Hugo" (Jipe moyo Hugo) wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Ivory Coast mjini Nantes.

Majeraha ya aina hiyo yanaweza kumweka mchezaji nje ya uwanja kwa hadi miezi 12, hali inayomaanisha Ekitike anaweza kuukosa sehemu kubwa ya msimu ujao.

HUG 01

Aonekana akitembea kwa fimbo Wimbledon

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alionekana kwenye viwanja vya Wimbledon akiwa amevalia suti ya kifahari ya Dolce & Gabbana, tai yenye michoro maalumu na akitumia fimbo kumsaidia kutembea kabla ya kuingia kutazama mechi katika eneo la wageni maalumu la Wimbledon Suite.

Muonekano wake umeonyesha kuwa anaendelea kupata nafuu hatua kwa hatua huku akirejea taratibu kwenye hali ya kawaida.

HUG 02

Anaendelea na programu maalumu ya mazoezi

Katika kipindi hiki cha mapumziko, Ekitike amekuwa Los Angeles, Marekani, akifanya mazoezi maalumu chini ya mtaalamu wa tiba ya viungo kutoka Ujerumani, Berengar Buschmann, ambaye aliwahi kufanya naye kazi walipokuwa Eintracht Frankfurt.

Wiki iliyopita, Buschmann alichapisha video ikimuonyesha Ekitike akifanya mazoezi mbalimbali ya kuimarisha misuli ya sehemu ya chini ya mguu, mazoezi ya ndani ya bwawa la kuogelea pamoja na mazoezi mepesi ya mpira.

Mapema wiki hii, mtaalamu huyo pia alishiriki video nyingine ikimuonyesha Ekitike akitembea bila kutumia kifaa maalumu cha kuvaliwa mguuni, hatua iliyotafsiriwa kuwa mafanikio makubwa katika safari yake ya kupona.

Katika maelezo ya video hiyo aliandika:"Kama umewahi kuvaa walking boot, unajua hisia hizi. Kuivua ni hatua muhimu, lakini kuona mwendo wa kutembea ukianza kurudi katika hali ya kawaida ni hatua nyingine kubwa. Safari bado inaendelea. Kila maendeleo yanapatikana kwa juhudi na uvumilivu."

HUG 03

Alikuwa tegemeo la Liverpool

Kabla ya kupata jeraha hilo lililokatisha msimu wake, Ekitike alikuwa mmoja wa wachezaji waliotoa matumaini ndani ya kikosi cha Liverpool, akifunga mabao 17 katika msimu uliokuwa na changamoto kwa miamba hiyo ya Anfield.

Sasa mashabiki wa Liverpool wataendelea kusubiri kwa hamu siku ambayo mshambuliaji huyo atarejea uwanjani akiwa fiti kuiongoza tena safu ya ushambuliaji ya Majogoo.