Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hojlund kuuzwa, Zirkzee kubaki

MAN UTD Pict

Muktasari:

  • Man United inataka kuboresha safu yake ya ushambuliaji kuongeza nguvu kwenye eneo hilo katika dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, hivyo ishu ya kunasa straika mpya ipo kwenye mipango yao.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imeripotiwa kuchukua uamuzi wa kumpiga chini Rasmus Hojlund, lakini Joshua Zirkzee atabaki kwenye kikosi hicho cha miamba ya Old Trafford.

Man United inataka kuboresha safu yake ya ushambuliaji kuongeza nguvu kwenye eneo hilo katika dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, hivyo ishu ya kunasa straika mpya ipo kwenye mipango yao.

Mastraika Hojlund na Zirkzee hawakuwa na kiwango bora msimu uliopita, wakifunga mabao 17 kwa pamoja katika mechi 105 walizocheza kwenye michezo yote. Man United ilitumia Pauni 72 milioni kumsajili Hojlund kutoka Atalanta mwaka 2023 na Pauni 36.5 milioni kumsajili Zirkzee kutoka Bologna mwaka 2024.

Wachezaji hao wawili wote walitazamiwa kuachana na miamba hiyo ya Old Trafford kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi, lakini kwa mujibu wa gazeti la Corriere dello Sport, Man United imeamua kubaki na Zirkzee na badala yake itampiga bei Hojlund.

Gazzetta dello Sport, kwa upande wake linafichua Inter Milan imeingia kwenye mazungumzo na Man United kuhusu mshambuliaji Hojlund. Na kwenye ripoti hiyo, Man United inataka ilipwe walau Pauni 38 milioni kwa straika huyo mwenye umri wa miaka 22, pesa ambayo itakuwa haraka kwa timu kulinganisha na pesa iliyotumika kumsajili.

Inter inaripotiwa kwenda kasi kwenye mpango wa kumsajili Hojlund na matumaini yao ya awali watamnyakua kwa mkopo wenye kipengele cha kumbeba jumla. Licha ya kwamba Man United inataka kumuuza kabisa straika huyo kwenye dirisha hili, lakini inaweza kukubali kumtoa kwa mkopo kama dili hilo litakuwa la pesa nzuri.

Straika Hojlund hivi karibuni aliulizwa kuhusu hatima yake kwenye kikosi hicho wakati akiwa kwenye majukumu ya soka la kimataifa na kikosi chake cha Denmark, alisema: "Nina mkataba hadi 2030, hivyo natarajia kuendelea kuichezea Manchester United. Najiandaa kwenda mapumzikoni na baada ya hapo, nitakuwa tayari kujitolea na kuwekekeza nguvu kwenye mipango iliyopo mbele."

Man United tayari imeshaongeza mshambuliaji mmoja kwenye kikosi chake badaa ya kutumia Pauni 62.5 milioni kunasa saini ya staa wa Wolves, Matheus Cunha. Cunha alifunga mabao 15 msimu uliopita akiwa na Wolves.