Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hii ni mechi ya kibabe Kombe la Dunia la Klabu

KIBABE Pict

Muktasari:

  • Real Madrid ilimaliza vinara kwenye Kundi H, ikivuna pointi saba katika mechi tatu, wakati Juventus ilimaliza namba mbili kwenye Kundi G, ikivuna pointi sita katika mechi tatu ilizocheza katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.

PHILADELPHIA, MAREKANI: MIAMBA miwili ya Ulaya, Real Madrid na Juventus itakumbana yenyewe kwenye hatua ya 16 bora ya fainali za Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani, usiku wa Jumanne, zikichuana kuwania tiketi ya kutinga kwenye robo fainali ambayo ina mkwanja mrefu.

Real Madrid ilimaliza vinara kwenye Kundi H, ikivuna pointi saba katika mechi tatu, wakati Juventus ilimaliza namba mbili kwenye Kundi G, ikivuna pointi sita katika mechi tatu ilizocheza katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Real Madrid ilibanwa kwenye mechi ya kwanza baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Al-Hilal, lakini ilishinda mechi zake zilizofuatia dhidi ya Pachuca na Red Bull Salzburg na hivyo kukamatia tiketi hiyo ya raundi ya 16 bora. Kikosi hicho cha Los Blancos sasa kipo chini ya kocha Xabi Alonso.

Hii itakuwa mechi ya kwanza kwa Real Madrid na Juventus kukutana tangu zilipomenyana kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2017-18, ambapo Old Lady ilishinda mechi hiyo kwa mabao 3-1 Hispania, lakini Los Blancos ilisonga mbele kwa jumla ya mabao 4-3.

Juventus, kwa upande wake ilikuwa vizuri kwenye mechi mbili za kwanza za makundi, ambapo iliichapa Al Ain 5-0 kabla ya kupata ushindi wa 4-1 dhidi ya Wydad AC. Baada  ya hapo, Juve ilikipiga na Manchester City na hapo ikakumbana na kipigo cha mabao 5-2 na hivyo kumaliza katika nafasi ya pili kwenye kundi na kujikuta ikikabiliwa na Real Madrid, kupambania nafasi ya kucheza robo fainali dhidi ya ama Borussia Dortmund au Monterrey.

Kwa ujumla wake, Juventus na Real Madrid zimekutana mara 21, ambapo miamba hiyo ya Hispania inaongoza ikipata ushindi mara 10 dhidi ya tisa, huku mara mbili tu zilitoka sare.

Staa wa Real Madrid, Kylian Mbappe, ambaye hajacheza mechi yoyote ya Kombe la Dunia la Klabu hadi sasa anaweza kuanzia kwenye benchi huku kocha Alonso akitamba na fomesheni ya 3-5-2.

Juventus inaweza kufanya mabadiliko ya kimfumo katika mechi hiyo ili iwe tofauti na kile kilichochapwa na Man City.

Mechi nyingine ya hatua ya 16 bora iliyochezwa alfajiri ya kuamkia Jumanne, Manchester City ilikuwa kwenye kasheshe zito la kukabiliana na miamba ya Saudi Arabia, Al-Hilal.

Vikosi vinavyotarajiwa;

Real Madrid: Courtois; Tchouameni, Rudiger, Huijsen; Alexander-Arnold, Bellingham, Guler, Valverde, F Garcia; Vinicius, G Garcia

Juventus: Di Gregorio; Savona, Kelly, Kalulu; Costa, Thuram, McKennie, Cambiaso; Conceicao, Kolo Muani, Yildiz