He! Arsenal yaajiri kocha wa mipira ya kurusha
Muktasari:
- Arsenal imekuwa wafalme wa mipira iliyokufa chini ya kocha Mikel Arteta kwa miaka kadhaa.
LONDON, ENGLAND: ARSENAL inataka iwe tishio zaidi kwenye mipira iliyokufa baada ya kumchukua gwiji wa mipira ya kurusha, Thomas Gronnemark.
Arsenal imekuwa wafalme wa mipira iliyokufa chini ya kocha Mikel Arteta kwa miaka kadhaa.
Miamba hiyo ya Emirates ni miongoni mwa timu zilizofunga mabao mengi kwa mipira hiyo Ligi Kuu England msimu huu ikilingana na Chelsea na Leeds United.
Lakini, kwenye mabao hayo hakuna hata moja lilifungwa kutokana na mpira wa kurushwa, hivyo Arteta anataka kumaliza tatizo hilo.
Arsenal imefanya mawasiliano na Gronnemark, ambaye ana umaarufu mkubwa kama mmoja wa makocha bora wa mipira ya kurusha duniani.
Gronnemark amefanya kazi na zaidi ya klabu 30, lakini alipata umaarufu mkubwa alipokuwa chini ya Jurgen Klopp huko Liverpool.
Liverpool ilinyakua ubingwa wa Ligi Kuu England kipindi cha Gronnemark alipokuwa katika timu hiyo na Klopp alisifu mchango wake.
Klopp amesema: “Niliposikia kuhusu Thomas, nilikuwa na uhakika wa asilimia 100 nataka kumwajiri. Tulimleta Thomas na alibadili ishu ya mipira ya kurusha.”
Arteta amesema Declan Rice atakuwa mtaalamu wa mipira ya kurusha kama ambavyo amekuwa hodari kupiga mipira ya friikiki.
Arteta amesema: “Kila kitu ni lazima kihusishwe. Nafahamu ni ubora gani alionao Declan...”