Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Harry Kane ashajua siku ya kubeba kombe

Muktasari:

  • Kane alianzishwa kwenye fowadi ya Bayern Munich wakati ilipotokea nyuma kushinda 3-1 dhidi ya VfB Stuttgart kwenye mikikimikiki ya Bundesliga, Ijumaa iliyopita.

MUNICH, UJERUMANI: TAJI la kwanza la Harry Kane kwenye maisha yake ya soka limeshafahamika atalibeba lini msimu huu.

Kane alianzishwa kwenye fowadi ya Bayern Munich wakati ilipotokea nyuma kushinda 3-1 dhidi ya VfB Stuttgart kwenye mikikimikiki ya Bundesliga, Ijumaa iliyopita.

Kwa bahati mbaya supastaa huyo wa England hakufunga wala kuasisti katika mechi hiyo, hivyo kubaki na mabao yake 21 na asisti nane kwenye ligi msimu huu.

Kwenye mechi hiyo, mabao matatu ya Bayern yalifungwa na Michael Olise, Leon Goretzka na Kingsley Coman, huku lile la kujifariji la Stuttgart lilifungwa na Angelo Stiller katika dakika ya 34 ya mchezo.

Lakini, hilo halimzuii Kane kuonyesha furaha yake juu ya ushindi wakati alipoandika kwenye Instagram: “Ni wakati bora kabisa! Ushindi wa aina yake! Kiwango bora kabisa cha uchezaji ugenini!!”

Ushindi huo uliifanya Bayern kujitanua kileleni kwenye msimamo wa Bundesliga kwa pointi 11 dhidi ya Bayer Leverkusen iliyopo nafasi ya pili, ambayo ilishinda 4-1 dhidi ya Eintracht Frankfurt, Jumamosi na kufanya pengo la pointi kuwa nane. Kwa pengo hilo la pointi, kuna uhakika Bayern itaweza kushikilia bomba kwenye mechi 10 zilizobaki na kubeba taji hilo la ubingwa wa ligi. Kama pengo la pointi nane litabaki lilivyo, basi Bayern inaweza kutangaza ubingwa Mei 3, itakapokipiga na RB Leipzig. 

Kuhusu taji jingine inaloweza kubeba Bayern msimu huu, lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya, straika Kane atakuwa na shughuli mbele ya Leverkusen, kwenye mchezo wa mtoano wa hatua ya 16 bora. Kwenye mbio za ubingwa wa Bundesliga, Bayern itahitaji ushindi kwenye mechi nane tu zijazo ili Kane abebe taji lake la kwanza kwenye maisha yake ya soka.