Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Harry Kane anaua tu, aweka rekodi hii

KANE Pict

Muktasari:

  • Kane amefunga mabao hayo 500 akiwa na Bayern, Tottenham na timu ya taifa ya England na kwa sasa yeye ndiye mchezaji kwanza kutoka England kufikisha idadi hiyo ya mabao.

MUNICH, UJERUMANI: STAA wa Bayern Munich, Harry Kane ameweka rekodi baada ya kufunga mabao mawili katika mechi ya Bundesliga dhidi ya Werder Bremen na kufikisha jumla ya mabao 500 tangu aanze kucheza soka la kulipwa.

Kane amefunga mabao hayo 500 akiwa na Bayern, Tottenham na timu ya taifa ya England na kwa sasa yeye ndiye mchezaji kwanza kutoka England kufikisha idadi hiyo ya mabao.

Fundi huyu mwenye umri wa miaka 32, msimu huu anaonekana kuwa wa moto sana, kwani hadi hadi sasa amefunga mabao 41 katika mechi 35 za michuano yote.

Kati ya mabao 500 hayo aliyofunga katika maisha yake ya soka hadi sasa, 100 yametokana na penalti, ikiwamo moja dhidi ya Bremen.

Nahodha huyu wa England tangu awasili Ujerumani akiwa na Bayern amepiga penalti 23 na zote ameweka kambani.

Kane ameweka historia ya kuwa staa wa kwanza wa England kufikisha mabao 500 ya katika mechi rasmi na kabla ya hapo tayari alikuwa mchezaji mwenye mabao mengi zaidi katika historia ya England baada ya kumpita Jimmy Greaves ya mabao 474 Desemba mwaka jana.

Huu ni msimu mwingine wa kushangaza wa kufunga mabao kwa Kane, ambaye tayari ana mabao 26 katika mechi 22 za Bundesliga na bado ana mechi 12 zaidi za kucheza hivyo, kuna uwezekano akaivunja rekodi yake ya msimu uliopita katika ligi na hata michuano ya kimataifa.