Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guehi, Rice hatarini kukosa robo fainali

ENGLAND Pict

Muktasari:

  • Guehi alipata majeraha madogo ya msuli wa nyuma wa paja baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mexico katika hatua ya 16 Bora kwenye Uwanja wa Azteca.

MIAMI, MAREKANI: ENGLAND imepata pigo jipya kuelekea robo fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Norway baada ya beki wa kati Marc Guehi kusubiriwa kufanyiwa tathmini ya mwisho saa chache Ijumaa ili kubaini kama atakuwa fiti kucheza dhidi ya Erling Haaland leo, Jumamosi.

Guehi alipata majeraha madogo ya msuli wa nyuma wa paja baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mexico katika hatua ya 16 Bora kwenye Uwanja wa Azteca.

Awali ilidhaniwa kuwa alikuwa amechoka misuli kutokana na mechi ngumu, lakini taarifa zinaeleza kuwa beki huyo wa Manchester City amepata maumivu ya misuli.

Hata hivyo, Guehi anaamini bado ana nafasi ya kucheza na anaendelea kupambana kuhakikisha anarejea kwa wakati.

Iwapo hataweza kufanya mazoezi na wenzake Ijumaa, nafasi yake ya kucheza dhidi ya Norway itakuwa mashakani.

Ingawa majeraha hayo hayajaonekana kuwa makubwa, kocha Thomas Tuchel hataki kuhatarisha hali ya mabeki wake hasa wakati England inajiandaa kumkabili mshambuliaji hatari wa Norway, Erling Haaland, ambaye tayari amefunga mabao saba katika mashindano haya.

ENG 04

Rice bado hajarudi mazoezini

Habari nyingine zisizofurahisha kwa England ni kwamba kiungo Declan Rice amekosa mazoezi kwa siku ya pili mfululizo kutokana na maradhi.

Rice alikuwa tayari akisumbuliwa na tatizo la neva lililoathiri misuli ya nyuma ya paja na sehemu ya chini ya mgongo, huku ugonjwa huo ukizidisha hali yake.

Kikosi cha England kimechukua tahadhari kuhakikisha ugonjwa huo hausambai kwa wachezaji wengine kambini.

ENG 03

James arejea kwa wakati

Habari njema kwa Tuchel ni kurejea kwa beki wa kulia Reece James, ambaye alifanya mazoezi kamili kwa mara ya kwanza tangu alipoumia hamstring kwenye sare ya bila kufungana dhidi ya Ghana.

Ingawa hakumaliza kipindi chote cha mazoezi, James anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Norway, mradi tu hatapata maumivu yoyote baada ya mazoezi hayo.

Kurejea kwake ni nafuu kubwa kwa England ambayo imekuwa ikikumbwa na matatizo katika nafasi ya beki wa kulia kutokana na majeraha na adhabu za wachezaji.

ENG 02

England yapungua chaguo safu ya ulinzi

Matatizo ya England yameongezeka baada ya Jarell Quansah kufungiwa mechi mbili kufuatia kadi nyekundu aliyopewa dhidi ya Mexico.

Aidha, Tino Livramento wa Newcastle aliumia misuli ya mguu kabla ya mashindano kuanza, hali iliyomlazimu Tuchel kumuita Trevoh Chalobah kuchukua nafasi yake.

Kutokana na majeraha na adhabu hizo, Djed Spence ndiye aliyebaki kuwa beki wa kulia wa asili katika kikosi hicho.

Endapo Guehi hatakuwa fiti, Tuchel atalazimika kuwategemea John Stones, Dan Burn au Chalobah kucheza katikati ya ulinzi.

ENG 01

Konsa: Stones alitaka kunipunguzia mzigo

Beki wa Aston Villa, Ezri Konsa, aliyelazimika kucheza beki wa kulia katika ushindi dhidi ya Mexico, amesema haikuwa kazi rahisi kubadili nafasi katikati ya mchezo.

“Kutokana na joto na kulazimika kubadili nafasi ukiwa pungufu ya mchezaji mmoja, haikuwa rahisi kabisa.”

Aliongeza kuwa ilibidi ajizoeshe haraka na majukumu mapya ya kuzuia mashambulizi kupitia pembeni.

“Dakika 10 za mwanzo zilikuwa ngumu kiakili, lakini nilibadilika na kuzoea hali hiyo.”

Konsa pia alimpongeza John Stones kwa kumtia moyo muda wote uwanjani.

“Hata aliniambia tubadilishane nafasi, lakini nilimwambia asiwe na wasiwasi, ningeweza kuendelea.”

Alimalizia kwa kusisitiza kuwa yuko tayari kucheza popote atakapopangiwa na kocha.

“Nitacheza nafasi yoyote ambayo kocha atanipa. Mradi tu niko uwanjani na ninalisaidia taifa langu, nitakuwa na furaha.”