Haaland akumbuka kesi ya Man City
Muktasari:
- Miamba hiyo ya Ligi Kuu England inakabiliwa na mashtaka 115 juu ya ukiukwaji wa mapato na matumizi, lakini sasa mashtaka hayo yalipanda hadi 130 kutokana na sababu nyingine za kiutawala.
MANCHESTER, ENGLAND: STRAIKA Erling Haaland anaamini Manchester City haitakumbana na adhabu yoyote kwenye mashtaka yanayoikabili ya kukiuka kanuni za mapato na matumizi kwenye kikosi hicho cha Etihad.
Miamba hiyo ya Ligi Kuu England inakabiliwa na mashtaka 115 juu ya ukiukwaji wa mapato na matumizi, lakini sasa mashtaka hayo yalipanda hadi 130 kutokana na sababu nyingine za kiutawala.
Man City imekuwa ikikanusha kutenda makosa yoyote katika kipindi cha miaka 14, huku kocha Pep Guardiola akiamini klabu hiyo haina hatia.
Straika Haaland alisaini mkataba mrefu wa miaka tisa na nusu Januari mwaka huu, akiamini timu hiyo haijafanya kosa lolote kama anavyoamini Guardiola.
Haaland, 25, anaamini mabosi wa Man City watakuwa hawafanya kosa lolote.
Alisema: “Nimezungumza na mabosi, na ninawaamini. Kilikuwa kipindi kigumu kwangu mimi kuanzia kukaa na mabosi na kuzungumza nao juu ya hilo, kwa sababu nikijua sikuhusika pia. Nadhani klabu inafahamu tunachokifanya.”