Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gundogan anabaki, De Bruyne ataamua

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Staa huyo wa Kijerumani atapatikana bure kabisa mwaka huu, kutokana na mkataba wake kufika ukomo Bayern Munich miezi michache kutoka sasa. Miamba hiyo ya Bundesliga ilijaribu kumpa dili jipya kiungo huyo ili abaki Allianz Arena bila mafanikio.

LONDON, ENGLAND: HABARI ndo hiyo. Arsenal imeanza mazungumzo ya kumsajili kiungo Joshua Kimmich, ikielezwa utakuwa usajili wa kibabe sana kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Staa huyo wa Kijerumani atapatikana bure kabisa mwaka huu, kutokana na mkataba wake kufika ukomo Bayern Munich miezi michache kutoka sasa. Miamba hiyo ya Bundesliga ilijaribu kumpa dili jipya kiungo huyo ili abaki Allianz Arena bila mafanikio.

Ilielezwa huko nyuma mabosi wa Bayern waliondoa mezani ofa yao baada ya mchezaji huyo kutaka mshahara wake upandishwe hadi Pauni 320,000 kwa wiki. Na sasa Arsenal inataka kutumia fursa kunasa huduma ya mchezaji huyo.

Ripoti kutoka Ujerumani, Arsenal imeshafanya mazungumzo ya kumnasa Kimmich, ambaye pia amekuwa akisikiliza ofa za klabu nyingine. Bayern bado ina matumaini kwamba mchezaji wao huyo atabaki, lakini pia kuna ofa za klabu nyingine kama za Paris Saint-Germain, Liverpool na Manchester City zinamtaka.

“Dili mpya? Ni wazi, hatuwezi kusubiri milele, lakini tunataka kumpa Joshua muda wa kutosha na tunafahamu ni mtu mwenye ukomavu mkubwa kwenye klabu ya Bayern Munich,” alisema bosi wa timu hiyo, Max Eberl.

Arsenal inamtaka kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30 ili akachukue mikoba ya Jorginho, ambaye mwisho wa msimu huu anatarajia kutimkia zake Brazil.

“Mkataba wangu upo hadi Juni na malengo yangu kwa sasa ni kufikiria tu mechi ijayokuja mbele. Sina cha kufikiria zaidi,” alisema Jorginho alipojaribu kuzungumzia hatima yake.

Jorginho aliongeza: “Kuna uwezekano wa kurudi Brazil, ndiyo kwa huko baadaye, hilo linawezekana. Kama nilivyosema, sijawahi kucheza soka la kulipwa Brazil hivyo itakuwa vyema kwenye kupata huo uzoefu. Hivyo, milango ipo wazi.”

Kimmich alijiunga na Bayern akitokea RB Leipzig mwaka 2015 na amechezea timu hiyo kwenye mechi zaidi ya 400. Ndani ya muda huo ameshinda mataji manane ya Bundesliga, Ligi ya Mabingwa Ulata mara moja, Kombe la Ujerumani mara tatu na mataji mengine. Kimmich pia ameichezea timu ya taifa ya Ujerumani mara 97 kwenye soka la kimataifa tangu alipoanza kuitumikia nchi yake mwaka 2016.