Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola kula za kichwa kwa Wirtz

Muktasari:

  • Man City ilionekana kuwa mstari wa mbele katika kufukuzia huduma ya kiungo huyo mchezeshaji wa Bayer Leverkusen, ambaye amekuwa akiwindwa na timu nyingi baada ya kuonyesha kiwango bora kabisa huko kwenye Bundesliga.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER City imepata pigo kwenye mpango wao wa kumsajili Florian Wirtz - ambaye wanadhani ni mrithi sahihi wa Kevin de Bruyne - baada ya mkali huyo kudai anataka kujiunga na Bayern Munich mwishoni wa msimu huu.

Man City ilionekana kuwa mstari wa mbele katika kufukuzia huduma ya kiungo huyo mchezeshaji wa Bayer Leverkusen, ambaye amekuwa akiwindwa na timu nyingi baada ya kuonyesha kiwango bora kabisa huko kwenye Bundesliga.

Wirtz alifunga mabao 10 na asisti 10 katika Bundesliga msimu huu, huku mabao sita akifunga kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na sasa anataka kuzifikisha juu kabisa zama zake za soka kwa kuhamia katika klabu kubwa.

Man City ilikuwa ikimtazama kama mchezaji sahihi wa kwenda kuvaa buti za De Bruyne huko Etihad, baada ya supastaa huyo wa Kibelgiji kutangaza ataachana na miamba hiyo ya jiji la Manchester mwishoni mwa msimu huu baada ya kuitumikia kwa miaka 10.

Man City iliamini itanasa saini yake baada ya Leverkusen kuvutiwa na kiungo James McAtee na kipa Stefan Ortega, ambao ni wachezaji wa wababe hao wa Etihad, jambo ambalo linaaminika lingeweka wepesi wa kupatikana kwa Wirtz.

Mabosi wa Leverkusen walikwenda Man City kuzungumzia wachezaji hao wawili, ambapo Wajerumani hao wanamwona McAtee kuwa na thamani ya Pauni 25 milioni, ambapo walikuwa wakiamini kwenye mazungumzo hayo, angehusika pia kiungo Wirtz.

Lakini, Man City inaripotiwa kupata pigo baada ya kiungo huyo wa Kijerumani, Wirtz kumwambia kocha wake Xabi Alonso anachotaka ni kwenda kujiunga na wapinzani wa Leverkusen kwenye Bundesliga, Bayern Munich.

Ripoti ya Sport Bild inafichua kwamba mpango wa kiungo huyo mwenye miaka 22 unawahuzunisha Man City, sambamba na Real Madrid, ambayo pia ilikuwa ikipiga hesabu za kunasa saini ya mchezaji huyo kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Kocha wa Bayern, Vincent Kompany sasa atawaambia mabosi wake kufanya haraka kwenda kunasa saini ya kiungo huyo.