Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola hofu tupu kwa straika Haaland

Pep Pict

Muktasari:

  • Haaland alitolewa dakika za mwisho kwenye mechi hiyo ambayo Man City ilishinda 4-0 dhidi ya Newcastle na straika huyo aliibua wasiwasi kama atakuwa fiti kukipiga na Real Madrid kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Jumatano.

MANCHESTER, ENGLAND: PEP Guardiola amekiri kupatwa na hofu kubwa baada ya straika Erling Haaland kuanguka uwanjani na kushikilia goti kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle United wikiendi iliyopita, lakini bosi huyo wa Manchester City kwa matumaini alisema "haikuwa mbaya sana kama nilivyodhani."

Haaland alitolewa dakika za mwisho kwenye mechi hiyo ambayo Man City ilishinda 4-0 dhidi ya Newcastle na straika huyo aliibua wasiwasi kama atakuwa fiti kukipiga na Real Madrid kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Jumatano.

Man City ilichapwa 3-2 katika mechi ya kwanza dhidi ya Madrid kwenye mchujo wa kuwania tiketi ya hatua ya 16 bora kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, Jumanne iliyopita. Hata hivyo, Guardiola anaamini Haaland atacheza.

Alipoulizwa kuhusu majeruhi ya Haaland, Guardiola alisema: "Kila mtu alishtuka wakati alipoanguka. Sikuzungumza naye wala sikuzungumza na madaktari, lakini natumaini atakuwa fiti. Pengine halikuwa tatizo baya sana kama tulivyodhani."

Bado haijafahamika tatizo la Haaland ni kubwa kiasi gani, lakini staa mpya wa Man City, aliyesajiliwa kwenye dirisha la Januari, Omar Marmoush, ataongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo endapo kama mkali huyo wa Norway atashindwa kucheza dhidi ya Madrid.

Marmoush alifunga hat-trick dhidi ya Newcastle na Guardiola amemwagia sifa za kutosha mshambuliaji wake huyo, akisema: "Marmoush alifanya vizuri Ujerumani (Eintracht Frankfurt). Mchezaji wa kiwango kama chake, mwenye kasi vile, nimefarijika amefunga. Kwenye lile eneo la mbele, alikuwa mzuri sana. Tunafahamu, siku si nyingi atakuwa mfungaji wa mabao ya kutosha, kwa sababu ni mmaliziaji mzuri."