Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola: Hawa Arsenal wana balaa

ARSENAL (1)
ARSENAL (1)

Muktasari:

  • Ukiweka kando pengo la pointi sita, Arsenal imekuwa haifungiki pia, huku Guardiola akitania kwamba anaamini siku moja miamba hiyo ya Emirates itaruhusu mpira kutinga kwenye nyavu zao.

MANCHESTER, ENGLAND: KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amekiri kwamba Arsenal haikamatiki kwa sasa wakati chama hilo la Mikel Arteta likiweka pengo la pointi sita kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Ukiweka kando pengo la pointi sita, Arsenal imekuwa haifungiki pia, huku Guardiola akitania kwamba anaamini siku moja miamba hiyo ya Emirates itaruhusu mpira kutinga kwenye nyavu zao.

Arsenal imekuwa moto kwenye mbio za ubingwa baada ya kuichapa Burnley, Jumamosi iliyopita, shukrani kwa mabao ya Viktor Gyokeres na Declan Rice kwenye ushindi wao wa 2-0. 
Mechi hiyo bila ya kuruhusu bao uwanjani Turf Moor ilikuwa ya nne kwenye Ligi Kuu England msimu huu, ambapo Arsenal imewadhibiti wapinzani wao kufunga dhidi yao.

Mara ya mwisho Arsenal kuruhusu bao ilikuwa Septemba 28, 2025, wakati Nick Woltemade wa Newcastle United alifunga kwenye kipindi cha kwanza, zaidi ya hapo, chama hilo la Arteta halijaruhusu tena bao. 

Safu yao ya ulinzi inatajwa kama miongoni mwa beki bora kabisa Ulaya kwa sasa, huku usajili wao uliofanywa kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi, limewaongezea nguvu zaidi.

Guardiola amesema: "Tupo nyuma kwa pointi sita dhidi ya Arsenal, ambao kwa sasa hawazuiliki na wanacheza soka maridadi. Hawaruhusu mabao, wameimarika sana, wanaweza kufunga katika mazingira na wachezaji wengi. Lakini, kama tukipambana kidogo na wachezaji wetu wengi wakianza kufunga na jinsi mechi zilivyo, tunaweza kushinda."

Man City imeshacheza na Arsenal na kuambulia pointi moja ugenini Emirates. Gabriel Martinelli aliifungia Arsenal bao la kusawazisha kuigomea Man City kushinda, lakini tangu hapo, miamba hiyo ya kocha Arteta imekuwa balaa kubwa, haifungwi kirahisi, imeruhusu mabao matatu tu.

Kwenye hilo, Guardiola amesema kwa kutania: "Natumaini Arsenal itaruhusu bao siku moja. Sio kitu rahisi kukabiliana nao."

Guardiola ameshuhudia kikosi chake kikirejea kwenye hali ya ushindi baada ya kuchapwa na Aston Villa walipoichapa Bournemouth uwanjani Etihad, Jumapili iliyopita. Straika Erling Haaland alifunga mara mbili katika mabao matatu yaliyofungwa na timu hiyo.

Guardiola alikosa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita ukibebwa na Liverpool, ikiwa ni mara ya tatu katika kipindi cha miaka tisa.