Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haaland afunga tena, Man City ikimaliza ukame wa ushindi ugenini

Muktasari:

  • Fowadi huyo wa Norway, ameonyesha kiwango cha ajabu msimu huu, akiwa amefunga mabao 24 katika mechi 14 za klabu na timu ya taifa, huku City ikipata alama tatu ugenini barani Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja.

VILLARREAL, HISPANIA: Erling Haaland ameendelea na rekodi yake ya kufunga alipofumania nyavu kwa mara ya 12 mfululizo, akiisaidia Manchester City kumaliza ukame wa ushindi ugenini kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuibuka na ushindi wa mabao 0-2 dhidi ya Villarreal, usiku wa Oktoba 21, 2025 mechi ikichezwa Estadi de la Ceràmica, Hispania.

Fowadi huyo wa Norway, ameonyesha kiwango cha ajabu msimu huu, akiwa amefunga mabao 24 katika mechi 14 za klabu na timu ya taifa, huku City ikipata alama tatu ugenini barani Ulaya kwa mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja.

Bao la Haaland katika mechi hiyo iliyochezwa Estadi de la Ceràmica, lilikuwa la mshambuliaji mwenye ujuzi zaidi, alipowahi kumpita beki Juan Foyth na kumalizia pasi ya chini kutoka kwa Rico Lewis.

City ilitengeneza nafasi mapema, Haaland alipiga kichwa pembeni ndani ya dakika mbili za kwanza, huku Jeremy Doku akimlazimisha kipa Luiz Junior kuokoa shuti la chini sekunde chache baada ya mechi kuanza.

Kikosi cha Pep Guardiola kilitawala kipindi cha kwanza, na nahodha Bernardo Silva aliongeza bao la pili kabla ya mapumziko kwa kichwa kizuri baada ya kupokea krosi ya Savinho.

Villarreal ilijaribu kurejea mchezoni kipindi cha pili, ambapo Pape Gueye alilazimisha Gianluigi Donnarumma kufanya kazi ngumu kwa shuti kali, na beki wa zamani wa Chelsea, Renato Veiga, akigonga mwamba mwishoni mwa mechi, lakini City ikaibuka na ushindi muhimu.

Man City imefikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tatu, imeshinda mbili na sare moja, imefunga mabao sita na kuruhusu mawili huku ikishika nafasi ya katika msimamo wa michuano hiyo.