Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Guardiola afunguka kusepa Man City

Muktasari:

  • Guardiola, 54, amekuwa kwenye kikosi cha Man City tangu 2016 na alisaini mkataba mpya kwenye klabu hiyo Novemba mwaka jana ambao utamfanya awepo Etihad hadi 2027.

MANCHESTER, ENGLAND: PEP Guardiola amefunguka kwamba atang'oka kwenye soka kwenda kumpumzika baada ya kuachana na Manchester City, lakini ameweka kando mpango wa kustaafu kazi yake ya ukocha.

Guardiola, 54, amekuwa kwenye kikosi cha Man City tangu 2016 na alisaini mkataba mpya kwenye klabu hiyo Novemba mwaka jana ambao utamfanya awepo Etihad hadi 2027.

Lakini, kocha huyo Mhispaniola, ambaye amejijengea umaarufu na kutambulika kama mmoja wa makocha bora kabisa wa muda wote, atakwenda mapumziko wakati mkataba wake utakapofika tamati.

Guardiola alifichua kwamba atahitaji mapumziko wakati atakapoamua kuachana na Man City, ambapo hadi hapo atakuwa amehudumu kwenye kazi hiyo ya ukocha kwa miaka 18.

Guardiola alisema: "Nataka watu wanikumbuke popote kule watakapokuwa. Baada ya mkataba wangu kumalizika hapa Man City, nitasimama. Sidhani kama nitastaafu, lakini nitakuwa na mapumziko. Jinsi gani nataka nikumbukwe, hilo bado silijui.

"Makocha wote wanataka kushinda ili wakumbukwe kwa kazi yao, lakini naamini mashabiki wa Barcelona, Bayern Munich na Man City wanatazama timu yangu inavyocheza. Kuna changamoto chache kama kocha. Sijui nini kitatokea huko mbele, lakini sijali kitu."

Hata hivyo, kocha huyo wa Man City hakufuta mpango wa kusaini mkataba mpya huko Etihad wakati huu utakapofika mwisho.

Alisema hivi: "Nitakapomaliza muda wangu hapa, mwaka mmoja, miaka miwili, miaka mitano, miaka mitano au miaka sita."

Guardiola ameshinda mataji 18 akiwa kocha wa Man City na hivyo kumfanya awe na rekodi ya kunyakua mataji 40 kwenye kazi yake hiyo ya ukocha akipita pia kwenye klabu za Bayern Munich na Barcelona.

Kati ya mataji yake makubwa aliyobeba ni pamoja na Ligi Kuu England mara sita, La Liga mara tatu na Bundesliga mara tatu, mataji 10 ya makombe ya ndani na Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tatu.

Sambamba na kubeba mataji hayo, kocha huyo ametambulika pia na Fifa, akishinda tuzo ya Kocha Bora wa Mwaka wa Fifa mara tatu tofauti. Guardiola ameweka rekodi nyingi ikiwamo kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England kwa misimu minne mfululizo na kuvuka pointi 100 kwenye Ligi Kuu England ndani ya msimu mmoja.