Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Giggs amweka rekodi

LISBON, Ureno KOCHA Alex Ferguson amemsifu kiungo wake mkongwe Ryan Giggs baada ya kufunga bao muhimu lililoisaidia Manchester United kupata pointi moja jijini Lisbon. Bao lake hilo limemfanya kufikisha idadi ya mabao 16 kwenye Ligi ya Mabingwa. Ameweka rekodi ya kucheza miaka 17 na pia Giggs mwenye miaka 37 ametegeneza rekodi mpya ya kuwa mchezaji mkubwa kufunga bao kwenye michuano hiyo. Kocha wa Fergie alisema: "Ni bao zuri la kiwango cha juu. "Mwanzoni alikuwa akicheza kama kiungo wa kati, lakini alipopokea mpira aliweza kuingia katikati na kutegeneza nafasi nyingi za hatari langoni kwa adui. "Bao lake ni zuri kwa sababu alichukua mpira kutoka pembeni na kuingia kati na kuwaacha viungo wao nyuma na kupiga shuti lililojaa wavuni." Giggs alifunga bao hilo dakika 42 kusawazisha lile la Oscar Cardozo aliloifungia kwanza Benfica. Fergie aliongeza: "Nafikiri mabao yote yalikuwa mazuri. Kijana Cardozo alifunga bao kwa ufundi mkubwa pia.