Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Giggs aanika ishu ya Rashford

Giggs Pict

Muktasari:

  • Rashford alikamilisha uhamisho wa mkopo kwenda Villa Januari mwaka huu ikiwa ni baada ya kupitia kipindi kigumu chini ya Ruben Amorim licha ya kuanza msimu vizuri akiwa ameshafunga mabao manne katika ligi hadi sasa.

MANCHESTER, ENGLAND: LEJENDI wa Manchester United, Ryan Giggs, amesema mshambuliaji wa timu hiyo, Marcus Rashford ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo Aston Villa lazima akubali kujitoa na kuupenda tena mpira wa miguu ili kufanikiwa na kurudi katika mstari.

Rashford alikamilisha uhamisho wa mkopo kwenda Villa Januari mwaka huu ikiwa ni baada ya kupitia kipindi kigumu chini ya Ruben Amorim licha ya kuanza msimu vizuri akiwa ameshafunga mabao manne katika ligi hadi sasa.

Msimu uliopita, Rashford alifunga mabao saba ya ligi, lakini Giggs anasema kwamba anavyoonekana kama ana "mzigo umemuelemea mabegani" na anatumai kuwa atabadilika na kurudi katika kiwango chake.

Giggs alikuwa miongoni mwa makocha Old Trafford wakati straika huyo alipoanza kupitia akademi ya timu hiyo.

Akizungumza na The Sun, Giggs alisema: "Man United wanahitaji wachezaji vijana wenye viwango, yeye alikuwa ni mmoja wao mwenye asili yao, na ilionekana kuwa yeye ndiye supastaa mkubwa anayefuata. Lakini kwa sababu mbalimbali, amekuwa na mafanikio kinyume na kile nilichofikiria kwamba anaweza kukifikia."

"Zaidi ya yote, yeye ni binadamu na haonekani kuwa ni mwenye furaha. Anaonekana kama ana dunia inamuelemea kwenye mabega yake. Na sijui kwa nini, kwa sababu ni tofauti kabisa na wakati ule nilipomuona na kumfundisha, hakuwa na mzigo unaomuelemea."

"Alikuwa anacheza kwa uhuru, aliipenda timu na alikuwa kijana mzur, lakini haonekani kuwa hivyo kwa sasa. Nina matumaini atapata ile hali aliyokuwa nayo miaka kumi iliyopita na asisahau kamwe kwamba hii ni kazi bora zaidi duniani.

"Unapaswa kufurahia maisha ya kucheza soka kwa sababu itamalizika haraka, lazima ujaribu kufurahia kila dakika yake. Anahitaji kucheza kwa uhuru na furaha iliyomfikisha hapa alipo sasa na ninatumai atafanya hivyo."