Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gernot Rohr aitahadharisha Nigeria kufuzu Kombe la Dunia

GERNOT Pict

Muktasari:

  • Nigeria inatarajiwa kumenyana na DR Congo katika mechi hiyo muhimu jijini Rabat leo Jumapili, Novemba 16, 2025 kwenye Uwanja wa Prince Héritier Moulay El Hassan.

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, Gernot Rohr, ametabiri matokeo ya fainali ya mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 kati ya Super Eagles na DR Congo.

Nigeria inatarajiwa kumenyana na DR Congo katika mechi hiyo muhimu jijini Rabat leo Jumapili, Novemba 16, 2025 kwenye Uwanja wa Prince Héritier Moulay El Hassan.

Ingawa Rohr anaiunga mkono timu yake ya zamani kuibuka na ushindi dhidi ya Leopards, kocha huyo mwenye uraia wa Ufaransa na Ujerumani ameonya kuwa DR Congo ina ubora unaoweza kuisumbua Nigeria.

Nigeria iliichapa Gabon 4-1 na kufuzu hatua ya fainali, huku DR Congo ikiitoa Cameroon kwa bao 1-0 na kutinga fainali.

MAY 02

Rohr anaendelea kuamini kuwa kikosi cha Nigeria kina uwezo mkubwa na kujitambua hasa kinapokuwa kwenye mechi muhimu kama hii ya leo, ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wengi wa soka barani Afrika.

“Kwangu ninaamini Nigeria ina nafasi kubwa ya kushinda, lakini hii haiiondolei ubora DR Congo, ninajua itakwenda uwanjani ikiwa na lengo la kuishangaza Super Eagles, hivyo niwasihi wachezaji wa Nigeria kuwa makini wakati wote licha ya ubora wao,” amesema Rohr.

“Ninawasisitiza lazima wacheze kwa nidhamu na tahadhari. Congo ni timu yenye nguvu kimwili na hatari sana katika mipira ya kutengwa, kama walivyoonyesha dhidi ya Cameroon. Nguvu yao ya kisaikolojia pia iko juu.”

GER 01

Ushindi kwa kikosi cha Eric Chelle utakuwa chachu ya hamasa kuelekea Fainali za Mataifa ya Afrika 2025 zitakazofanyika Morocco. Lakini kipigo kitavunja matumaini ya safari  yao ya kurejea kwenye michuano mikubwa ya soka duniani baada ya kuikosa nafasi hiyo mwaka 2022.

Benin, timu inayofundishwa na Rohr, itamenyana na DR Congo katika mchezo wao wa kwanza wa fainali za mataifa ya Afrika AFCON 2025, na kocha huyo amesema atatazama mchezo wa leo Jumapili, ili kuendelea kuwafahamu wapinzani wake.