Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Desabre atuma salamu Super Eagles, asisitiza kukiwasha

DESABRE Pict

Muktasari:

  • Leopards iliishangaza Cameroon maarufu Simba Wasiofungika kwa ushindi wa bao 1–0 katika Uwanja El Barid mjini Rabat, Morocco jana Alhamisi, Novemba 13, 2025 na kutinga hatua ya fainali ya mchujo wa Kombe la Dunia 2026.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya DR Congo maarufu Leopards, Sébastien Desabre, amesisitiza kuwa timu yake ina ubora wa kuifunga ‘timu bora Afrika’ Nigeria, hivyo amejipanga kwa mpambano huo wa mchujo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Leopards iliishangaza Cameroon maarufu Simba Wasiofungika kwa ushindi wa bao 1–0 katika Uwanja El Barid mjini Rabat, Morocco jana Alhamisi, Novemba 13, 2025 na kutinga hatua ya fainali ya mchujo wa Kombe la Dunia 2026.

Desabre amesema kwa kushirikiana na benchi lake la ufundi atakiandaa vizuri kikosi chake kuelekea kwenye mechi hiyo dhidi ya Super Eagles, itakayopigwa keshokutwa Jumapili, Novemba 16, 2025 ili kufanikisha azma ya kuibuka kidedea na kuendelea na harakati za kusaka tiketi ya Kombe la Dunia 2026.

Amesema anatambua Super Eagles ina kikosi bora kwa sasa, na huenda ikawa na timu bora barani Afrika katika kipindi hiki, lakini hilo halimtishi, kwani amejipanga kutumia mbinu nyingi ili kuibuka na ushindi.

CHELE Pict

“Nigeria bado ni bora barani Afrika. Tunajua bado tuna nafasi ya kuongeza ubora wetu tunapokutana na timu zilizo juu yetu kwenye viwango vya FIFA, kwa hiyo tutajiandaa vizuri ili kufanikisha lengo la kushinda mechi hiyo ” amesema Desabre.

MAY 02

“Tunayo timu yenye wachezaji wenye uzoefu mkubwa. Kile tunachokijenga hakikutokea kwa siku moja. Itakuwa mechi ya aina tofauti kabisa. Lolote litakalotokea, tutapambana kwa nguvu zetu zote. Nina uhakika tutashinda,” ameongeza kocha huyo kutoka Ufaransa.

DR Congo ilianza kampeni yake ya kufuzu Kombe la Dunia 2026 kwa umahiri na nidhamu chini ya kocha Sébastien Desabre. Katika Kundi B, Leopards ilifanya vizuri sana, ikishindana vikali na Senegal.

Moja wa matokeo muhimu kwenye mechi za mchujo za Kundi B ilikuwa ushindi wa 2–0 dhidi ya Mauritania kwenye Uwanja Nouadhibou, ambapo Charles Pickel aliifungia DR Congo bao la mapema na Fiston Mayele akaongeza la ushindi. Hii iliisaidia Leopards kuongoza Kundi B na kudhibiti hatma yao ya kufuzu kabla ya kuangukia kwenye mechi za mchujo.

Hata hivyo, safari ya Leopards haikukosa changamoto, kwani ilikumbana na upungufu wa mabao ya kufunga dhidi ya Senegal, ikipoteza mechi kwa kufungwa 2–3 nyumbani licha ya kuongoza kwa mabao mawili kupitia Bakambu na Wissa.

Mwishoni mwa mechi za mchujo hatua ya makundi, DR Congo ilibaki kuwa miongoni mwa timu zilizopata nafasi, ambapo ilipangwa kukutana na Cameroon iliyochezea kichapo cha 1-0, jana Alhamis, Novemba 13, 2025.