Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Geremi Njitap ampa maua yake Cole Palmer akimfanisha na Lampard

NJITAP Pict
NJITAP Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa mchezaji huyo wa zamani wa kikosi cha Cameroon, amesema wawili hao ni wafungaji bora, ingawa Palmer ni mchezaji wa kushambulia zaidi.

Kiungo wa zamani wa Chelsea, Geremi Njitap, amemlinganisha gwiji wa klabu hiyo, Frank Lampard na kinda anayetamba kwa sasa, Cole Palmer.

Kwa mujibu wa mchezaji huyo wa zamani wa kikosi cha Cameroon, amesema wawili hao ni wafungaji bora, ingawa Palmer ni mchezaji wa kushambulia zaidi.

Amesema Palmer amekuwa mchezaji wa kiwango cha kushangaza tangu alipojiunga na The Blues akitokea Manchester City mwaka 2023, hivyo anatarajia mambo mengi kutoka kwake kutokana na umri mdogo alionao.

NJITA 01

Mchezaji huyo wa kimataifa wa England, tayari ameshatwaa baadhi ya mataji akiwa na Chelsea, ikiwemo Kombe la Dunia la Klabu (FIFA Club World Cup).

Akizungumza na FourFourTwo, Njitap amesema: “Frank Lampard na Cole Palmer wote ni wafungaji wa mabao. Wanaweza kufunga wakati wowote ndani ya mchezo. Ukiangalia jinsi Frank alivyokuwa akicheza, alikuwa namba nane, mwenye sifa ya kucheza ‘box to box’.

“Palmer ni mchezaji wa kushambulia zaidi, lakini ana ubora mkubwa wa kiufundi. Palmer alikuwa na kiwango cha kushangaza wakati wa mechi ya fainali ya Kombe la Dunia la Klabu. Nilishangaa sana. PSG ilikuwa timu ya kuogopwa, ilikuwa inashinda kila kitu. Lakini, Chelsea ilishinda kwa kishindo.”