Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gabriel Martinelli, Isabella wanalitaka Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Ikiwa ni mara yake ya pili kushiriki michuano hiyo, ndoto ya kushinda taji la Kombe la Dunia haipo tu kwa Martinelli na mashabiki wa Brazil pekee, bali pia na kwa mchumba wa mchezaji huyo, Isabella Rousso, mzaliwa wa Rio De Janeiro.

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Gabriel Martinelli, 24, ni sehemu ya kikosi cha Brazil kinachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia 2026 na alicheza mchezo wa kwanza dhidi ya Morocco akiingia kutokea benchi katika mechi hiyo iliyomalizika kwa matokeo ya 1-1.

Ikiwa ni mara yake ya pili kushiriki michuano hiyo, ndoto ya kushinda taji la Kombe la Dunia haipo tu kwa Martinelli na mashabiki wa Brazil pekee, bali pia na kwa mchumba wa mchezaji huyo, Isabella Rousso, mzaliwa wa Rio De Janeiro.

Tunasema hivyo kwa sababu Isabella amekuwa mmoja wa watu muhimu sana katika maisha ya Martinelli akimuunga mkono tangu hatua za awali kabisa katika safari yake ya soka hadi sasa anapotambulika na wengi kama mmoja wa mchezaji mkubwa wa kimataifa.

Mathalani katika Kombe la Dunia la 2022 huko Qatar, Isabella alikwenda kumuunga mkono Martinelli pamoja na timu ya taifa ya Brazil, mabingwa wa michuano hiyo kwa mara tano na taji la mwisho walibeba mwaka 2002 nchini Japan.

Huko Qatar, Martinelli aliiwakilisha vizuri Brazil kwenye mashindano hayo na alicheza mechi tatu. Hata hivyo, ingawa hakuanza michezo mingi, alitoa mchango wake alipohitajika kufanya hivyo chini ya Kocha Adenor Bacchi maarufu kama Tite.

Hata hivyo, safari ya Brazil kwenye Kombe la Dunia 2022 iliishia robo fainali baada ya kuondolewa na Croatia kwa mikwaju ya penalti na sasa ni wakati mwingine kwa Martinelli kumpa mchumba wake, Isabella taji hilo maana ana kiu nalo.

Lakini Isabella si shabiki wa Martinelli tu akiwa na uzi wa Brazil, bali hufanya hivyo pia anapokuwa akiichezea klabu yake ya Arsenal na mara nyingi ameonekana katika Uwanja wa Emirates akiwa amevalia jezi ya Arsenal yenye jina na namba ya Martinelli mgongoni.

Martinelli alipofunga bao dhidi ya Manchester City mnamo Septemba 2025, wawili hao walisherehekea pamoja kwenye mitandao ya kijamii. Sababu kusherehekea pamoja ni Isabella alitabiri Martinelli angefunga siku hiyo, kwa mujibu wa video waliyoposti.

Mashabiki wengi walivutiwa na uelewa wa Isabella kuhusu soka, mmoja aliandika: Anajua soka. Huyu ndiye mfano wa mpenzi anayejua nini maana ya kumuunga mkono mtu wale.... Kila mwanamume anahitaji mwanamke kama huyu.

Wawili hao wamekuwa wakionekana katika maeneo mbalimbali maarufu jijini London, England, huku uhusiano wao ukivutia mashabiki wengi wa soka, ila bado hawajafunga ndoa wala kujaliwa kupata mtoto.

Ingawa haijulikani wawili hao walikutana lini na wapi hasa, lakini taarifa za uhakika ni Isabella kwa sasa anasomea udaktari huku akiendelea kujenga ushawishi katika mitandao ya kijamii na tayari ana wafuasi (followers) zaidi ya 232,000 katika ukurasa wake wa Instagram.

Hivyo Isabella anaendelea na masomo ya udaktari, jambo linaloonyesha ana ndoto ya kuwa daktari siku moja. Alisoma nchini Brazil kabla ya kuendelea na safari yake ya elimu akiwa London, ambako anaishi pamoja na Martinelli.

Mrembo huyo mara kwa mara huonyesha maisha yake ya masomo ya udaktari kupitia ukurasa wake wa Instagram. Akiwa hayupo masomoni, anaishi maisha ambayo wake na wapenzi wengi wa mastaa wa soka (WAGs) huyafurahia.

Mbali na masomo ya udaktari, Isabella pia anapenda sana kuchora na hutumia muda mwingi katika kipaji hicho. Kusafiri sehemu mbalimbali duniani ni jambo analolipenda sana mrembo huyo, mathalani mwaka 2022 kipindi cha majira ya joto, Isabella na Martinelli walitembelea nchi yao na walitumia muda mwingi katika kisiwa kizuri cha Fernando de Noronha, pia walienda Dubai na kupiga picha mbele ya jengo la Burj Al Arab.

Wawili hao wamekuwa pamoja tangu kipindi ambacho Martinelli anacheza soka Brazil kabla ya kuhamia London kujiunga na Arsenal mwaka 2019 akitokea klabu ya Ituano FC ya nchini kwao.

Mnamo Machi 2025, walitangaza rasmi kuwa wamechumbiana, jambo lililowafurahisha mashabiki wengi.