Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gabriel majanga Arsenal

Muktasari:


  • Gabriel alianza dhidi ya West Ham juzi na kuifungia timu yake bao la kuongoza akimalizia kwa kichwa kona ya Bukayo Saka katika mechi ambayo Gunners walitoa kipigo kizito cha 5-2 kwa mahasimu wao wa mji mmoja.

LONDON, ENGLAND: VICHWA vinawauma Arsenal wakijiuliza itakuwaje baada ya beki lao la kazi Gabriel kuumia huku mbele yao wakikabiliwa na mechi kubwa dhidi ya Manchester United keshokutwa Jumatano.

Gabriel alianza dhidi ya West Ham juzi na kuifungia timu yake bao la kuongoza akimalizia kwa kichwa kona ya Bukayo Saka katika mechi ambayo Gunners walitoa kipigo kizito cha 5-2 kwa mahasimu wao wa mji mmoja.

Lakini, alidumu uwanjani kwa dakika 45 tu kabla ya Mbrazili huyo kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Jakub Kiwior baada ya kupigwa ngumi ya usoni na kipa Lukasz Fabianski, faulo iliyozaa penalti na bao.

Hata hivyo, wakati akizungumza na wanahabari baada ya mechi ya West Ham, Arteta alithibitisha  kutolewa kwa Gabriel kulitokana na majeraha aliyoyapata wakati mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Sporting CP na si kutokana na kupigwa ngumi na Fabianski.

“Inatokana na majeraha aliyoyapata mapema mjini Lisbon,” alisema Arteta. “Alifanya vyema kuwa sehemu ya kikosi leo (juzi). Lakini baada ya kuongoza 5-2 na hali aliyokuwa akijisikia, tukaamua kumtoa.”

Gabriel si nyota pekee wa Arsenal aliyetolewa mapema katika ushindi huo mnono juzi. Saka na Riccardo Calafiori pia walitolewa, na kuongeza hofu kuhusu upana wa kikosi cha Arsenal katika kipindi hiki cha mechi nyingi mfululizo. Saka, ambaye mapema alifunga penalti ya bao la tano la Arsenal, alihitaji matibabu baada ya kugongana na Emerson lakini kocha Arteta alisema: “Yuko fiti.”

Kuhusu Calafiori, Arteta alisema alimpumzisha ili asijitoneshe goti lake.

“Amekuwa akipambania goti lake kwa wiki kadha, alikuwa na jeraha kubwa la goti, lakini sasa anaendelea hivyo ni lazima tudhibiti dakika anazocheza uwanjani.”