Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gabriel Jesus arejeshwa kikosini, Arsenal ikijiandaa na Club Brugge

Muktasari:

  • Jesus anachukua nafasi ya Max Dowman, ambaye alipata majeraha ya kifundo cha mguu wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika bila mashabiki dhidi ya Manchester United mwishoni mwa wiki iliyopita.

Arsenal wametangaza kuwa Gabriel Jesus ameongezwa kwenye kikosi cha Ligi ya Mabingwa Ulaya kuanzia sasa.

Jesus anachukua nafasi ya Max Dowman, ambaye alipata majeraha ya kifundo cha mguu wakati wa mchezo wa kirafiki uliofanyika bila mashabiki dhidi ya Manchester United mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mwezi uliopita, kijana huyo mwenye umri wa miaka 15 alikuwa mchezaji mdogo zaidi kuwahi kucheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya alipoingia uwanjani katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Slavia Prague, lakini sasa hatakuwa tena na sifa ya kucheza hadi hatua ya makundi kutamatika.

Wakati huohuo, Jesus ambaye pia alicheza kwenye mchezo huo wa mazoezi, yupo na kikosi kinachosafiri kwenda kukutana na Club Brugge kesho jioni.

Mara yake ya mwisho kucheza mechi ya Ulaya ilikuwa Desemba 2024, alipocheza katika ushindi wa nyumbani wa 3-0 dhidi ya Monaco. Awali aliachwa kwenye kikosi kutokana na jeraha la goti alilopata Januari 2025, hivyo kurejea kwake kutamfurahisha na bila shaka atapigania kupata nafasi ya kucheza nchini Ubelgiji.

Kocha Mikel Arteta anatarajia kutoa taarifa ya kikosi kitakachokwenda Ubelgiji kucheza mechi hiyo atakapoongea na wanahabari, lakini iliripotiwa mapema kuwa Declan Rice na Leandro Trossard wana nafasi ndogo ya kusafiri, huku kwa mara nyingine William Saliba akikosekana mazoezini.