Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Florian Wirtz atua Liverpool kwa Sh400 bilioni

WIRTZ Pict

Muktasari:

  • Liverpool imevunja benki kupata huduma ya mkali huyo, ilipolipa Pauni 116.5 milioni, ikiwa ni zaidi ya Sh 413 bilioni ili kumng’oa staa huyo kutoka Bayer Leverkusen.

LIVERPOOL, ENGLAND: RASMI sasa, kiungo wa Kijerumani, Florian Wirtz ni mchezaji mpya wa Liverpool na mwenyewe amefichua anataka kushinda kila taji huko Anfield.

Liverpool imevunja benki kupata huduma ya mkali huyo, ilipolipa Pauni 116.5 milioni, ikiwa ni zaidi ya Sh 413 bilioni ili kumng’oa staa huyo kutoka Bayer Leverkusen.

Ada hiyo ya uhamisho imevuka ile Pauni 115 milioni iliyolipa Chelsea kupata huduma ya kiungo wa Brighton, Moises Caicedo, Agosti 2023.

Liverpool ilishinda vita kali kutoka kwa klabu za Bayern Munich, Manchester City na Real Madrid katika mchakamchaka huo wa kunasa saini ya Wirtz, 22.

Wirtz alisema: “Najisikia furaha na najivunia. Hatimaye hii kitu imekwisha na nilikuwa naisubiri kwa muda mrefu – tumekamilisha na nina furaha sana. Nafurahia kuanza zama mpya.

“Hili ni jambo kubwa kwa maoni yangu, nataka kuwa na kitu kipya kabisa - kuondoka kwenye Bundesliga na kuhamia Ligi Kuu England. Ningependa kushinda kitu kila mwaka, tuwajibike kwa sababu tunataka kufanikiwa. Msimu uliopita walishinda Ligi Kuu England, lengo langu ni kushinda tena taji hilo na kwenda mbali kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hayo ndiyo malengo yangu.”

Staa huyo wa kimataifa wa Ujerumani anajiandaa kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa kwenye Ligi Kuu England baada ya kutua Anfield. Kinachoripotiwa ni amesaini mkataba utakaomshuhudia akilipwa Pauni 245,000 kwa wiki.

Hiyo ina maana atakuwa analipwa Pauni 12.7 milioni kwa mwaka, karibu mara 12 kwa kulinganisha na alivyokuwa akilipwa huko Leverkusen.

Kwa maana hiyo, Wirtz atakuwa na uhakika wa kuvuna Pauni 10.2 milioni kwa kila mwaka, huku kiasi kingine kitalipwa kulingana na bonasi ya kufanya vizuri ndani ya uwanja.

Hilo linamfanya Wirtz kuwa mchezaji namba tatu kwa mshahara mkubwa Liverpool, baada ya Mohamed Salah na Virgil van Dijk, ambao kila mmoja analipwa Pauni 400,000 kwa wiki.

Aliongeza: “Nitaona jinsi nitakavyocheza hapa. Natumaini nitakuwa kwenye ubora wangu. Nilizungumza na wachezaji waliowahi kucheza hapa na waliniambia ni mahali pazuri kwangu na uwanja pia ni mzuri, nitafurahia. Nasubiri kwa hamu kucheza mechi yangu ya kwanza.”