Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fifa yazipa ahueni klabu kuelekea AFCON

Muktasari:

  • Michuano ya Afcon itaanza Desemba 21 huko Morocco na kuna mastaa kibao wa Ligi Kuu England watakwenda kukipiga katika mikikimikiki hiyo.

LONDON, ENGLAND: KLABU za Ligi Kuu England ikiwamo Manchester United na Liverpool zimepata mzuka mpya baada ya FIFA kutoa utaratibu mwingine zinaweza kubaki na mastaa wao kwa wiki zaidi kabla ya kuwaruhusu kwenda kuungana na timu zao za taifa kwa ajili ya Afcon 2025.

Michuano ya Afcon itaanza Desemba 21 huko Morocco na kuna mastaa kibao wa Ligi Kuu England watakwenda kukipiga katika mikikimikiki hiyo.

FIFA imesema klabu haziruhusiwi kuachia wachezaji wake mapema kwa ajili ya michuano hiyo hadi Desemba 15. Hiyo itakuwa wiki moja zaidi ya ilivyokuwa awali.

Hiyo ina maana wachezaji akiwamo Mohamed Salah watakuwapo kwenye mechi za Ligi Kuu England katika wikiendi ya Desemba 13 hadi Desemba 14.

Kocha wa Liverpool, Arne Slot, alisema asubuhi ya Jumanne iliyopita: “Ataondoka Desemba 15.” Bosi huyo wa Kop aliongeza: “Kwa namna mambo yalivyokuwa, kulikuwa na mawasiliano ya pande zote tatu, mchezaji, klabu na nchi. Hakuna jipya. Lakini, FIFA ilisema Desemba 15 ni siku ya mwisho kwa wachezaji kuruhusiwa.”

Ruhusa hiyo bado inatazamwa kama itawasaidia Man United kuwatumia mastaa wake Bryan Mbeumo, Amad na Noussair Mazraoui kutumika kwenye mechi dhidi ya Bournemouth, Desemba 15.

Hata hivyo, si Liverpool na Man United pekee zitakazonufaika na jambo hilo. Klabu ya Ligi Kuu England ambayo ingeathirika pakubwa kutokana na michuano hiyo ya Afcon 2025 ni Sunderland.

Sunderland ina wachezaji saba wanaotazamiwa kwenda kucheza kwenye michuano hiyo ya Afcon 2025, hivyo itakuwa na nafasi ya kuwatumia wachezaji wao hadi kwenye mechi ya Wear-Tyne Derby dhidi ya Newcastle United, itakayopigwa Desemba 14.

Timu tatu ambazo hazitakuwa kwenye madhara makubwa kutokana na fainali hizo za Afcon ni Arsenal, Chelsea na Leeds United. Timu hizo hazina mchezaji yeyote kwenye vikosi vyao ambao wataondoka kurudi Afrika kwenda kusitumikia timu za taifa katika michuano hiyo.

Alipozungumza kabla ya mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya Everton wiki iliyopita, kocha wa Man United, Ruben Amorim alisema uongozi wa klabu hiyo unapambana kubaki na wachezaji wake kwenye timu kwa muda mrefu kwa kadri inavyowezekana kabla ya kuanza kwa Afcon 2025.

“Tuna sheria zetu, lini wakati wakati wa kuwaachia wachezaji, hivyo tusubiri tuone,” alisema.

“Tunafanya kazi yetu ya kujaribu kubaki na wachezaji wetu wiki kadhaa mbele, lakini hilo halipo kwenye uwezo wetu. Yatupasa kuheshimu hilo, lakini tutajaribu kufanya kila tunachokiweza kuilinda klabu, kuwalinda wachezaji na kuilinda timu ya taifa.

“Kwenye ishu hii tayari tumeshajua kitu, lakini ni fursa kwa wachezaji wengine. Tuna wachezaji pia wa umri wa chini ya miaka 21, tunataka kuwapatia ujumbe huu waufahamu. Lakini, ukweli utabaki kuwa palepale kwa sababu Amad, Mazraoui na Mbeumo ni wachezaji muhimu kwenye timu yetu na hatuna kikosi kipana. Lakini, akademia yetu kwa wakati huu itakuwa tayari.”

Michuano hiyo ya Afcon 2025 itaanza Desemba 21 na wenyeji Morocco watakipiga na Comoros. Fainali ya michuano hiyo itafanyika Januari 18.