Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Falcao amtesa Abramovich

LONDON, England BILIONEA wa Chelsea, Roman Abramovich ameitaka klabu hiyo kufanya kila linalowezekana kumsajili Radamel Falcao ifikapo Januari mwakani. Abramovich amesema yuko tayari kutoa kiasi cha Paundi 46 milioni. Mmiliki huyo wa Chelsea, amemtaja mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia, kama nyota mpya ajaye duniani kwa sasa na angependa atue dimba la Stamford Bridge. Mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid ameonyesha nia ya kutaka kujiunga na klabu hiyo tangu enzi za Kocha Andre Villas-Boas. Mabosi wa Chelsea wanaamini wanaweza kukamilisha dili la usajili kutoka klabu ya Madrid, ambayo imeonyesha nia ya kutaka kumuuza London labda kikwazo kiwe kiasi cha pesa. Chelsea itajaribu kufanya mazungumzo ili bei yake ishuke na hiyo ni kwa sababu ya hamu kubwa ya Abramovich kumwona Falcao akivaa jezi za rangi ya Blue. Falcao alijiunga na Madrid akitoka Porto kwa ada ya uhamisho ya Paundi 35 milioni mwaka jana. Chelsea, mabingwa wa Ulaya na wanaoongoza Ligi Kuu England kwa sasa, walitumia kiasi cha Paundi 60 milioni kuwasajili Eden Hazard, Oscar na Victor Moses msimu uliopita, lakini wanaonekana kuwa tayari kumwaga kiasi kingine cha pesa kumsajili Falcao. Pamoja na kufanya usajili mzuri msimu uliopita, Kocha Roberto Di Matteo hakufurahishwa baada ya klabu hiyo kushindwa kumsajili mshambuliaji wa kati. Fernando Torres ndiye mshambuliaji chaguo la kwanza la Chelsea msimu huu, akifunga mabao sita katika mechi 12. Di Matteo bado anaendelea kumtegemea Torres hivyo, kuja kwa Falcao kutamfanya kujivunia zaidi safu ya ushambuliaji Stamford Bridge. Falcao aliifunga Chelsea mabao matatu katika ushindi wa mabao 4-1 walipata wakati wa mechi Kombe la Super. Katika msimu wake wa kwanza Ligi Kuu Hispania, Falcao alifunga mabao 24, na sasa ameshakwamisha wavuni mabao nane akichuana vikali na Cristiano Ronaldo na Lionel Messi. Hata hivyo Chelsea huenda ikakumbana na ushindani mkubwa kumwania mchezaji huyo, kwani klabu ya Manchester City nayo inamfuatilia kwa karibu.