Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fainali Carabao... Huku Salah, kule Isak

Carabao Pict

Muktasari:

  • Utamu wa mechi hiyo ni kwamba Liverpool haijapoteza mechi kati ya 25 ilizocheza nyumbani dhidi ya Newcastle kwenye michuano yote. Na kwenye hilo, Liverpool imefunga walau mabao mawili katika mechi 10 kati ya 11 ilizocheza na Newcastle kwenye michuano yote. Kazi ipo.

LONDON, ENGLAND: MAMBO iko Wembley. Ndicho unachoweza kusema, wakati Liverpool itakapokipiga na Newcastle United kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Ligi, Jumapili.

Utamu wa mechi hiyo ni kwamba Liverpool haijapoteza mechi kati ya 25 ilizocheza nyumbani dhidi ya Newcastle kwenye michuano yote. Na kwenye hilo, Liverpool imefunga walau mabao mawili katika mechi 10 kati ya 11 ilizocheza na Newcastle kwenye michuano yote. Kazi ipo.

Baada ya kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mikwaju ya penalti dhidi ya PSG, hiyo ina maana kwamba kocha Arne Slot na kikosi chake cha Liverpool amebakiza mataji mawili ya kushindania katika msimu wake wa kwanza likiwamo hilo Kombe la Ligi, ambalo fainali yake inapigwa Jumapili.

Hata hivyo, Newcastle imepanga kuiduwaza Liverpool, wakati kikosi hicho cha kocha Eddie Howe, kitakaposaka taji lake la kwanza tangu msimu wa 1954/55 kilipobeba Kombe la FA. Katika mechi sita zilizopita baina ya timu hizo, Newcastle haijashinda hata moja, huku Liverpool ikipata ushindi kwa asilimia 84 na asilimia 16 ni sare. Lakini, hii ni fainali na chochote kinaweza kutokea.

Kwenye mchezo huo, Newcastle inapaswa kumchunga Mohamed Salah, ambaye amehusika kwenye mabao 18 katika mechi 16 dhidi yao akiwa na kikosi cha Liverpool, ambapo amefunga mabao 10 na kuasisti mara nane.

Katika rekodi ya mechi zote ilizokutanisha miamba hiyo, Liverpool imeshinda mara 93, Newcastle imeshinda mara 49 na sare ni 45.

Kwenye mechi hizo, Liverpool imefunga mabao 333, wakati Newcastle yenyewe imefunga mabao 223, ikiwa ni tofauti ya mabao 110. Wakati Liverpool ikitamba na Mo Salah, Newcastle yenyewe inaamini Alexander Isak atafanya maajabu yake ndani ya uwanja na kuipa timu hiyo taji lake la kwanza baada ya miaka mingi kupita.

Timu hizo zimefika fainali ya Kombe la Ligi baada ya kuzichapa klabu za London kwenye nusu fainali, ambapo Liverpool ilipenya kwa kupata ushindi mbele ya Tottenham Hotspur, wakati Newcastle iliisukuma nje ya mikikimikiki hiyo Arsenal baada ya kuichapa kwenye mechi zote mbili.


Vikosi vinavyotarajiwa;

Liverpool: Kelleher; Robertson, Van Dijk, Konate, Quansah; Mac Allister, Gravenberch, Szoboszlai; Diaz, Jota, Salah.

Newcastle: Pope; Livramento, Burn, Schar, Trippier; Joelinton, Tonali, Guimaraes; Barnes, Isak, Murphy.