Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Eti Saka, Saliba, Gabriel hawatasaini tena

Muktasari:

  • Arsenal imeweka matumaini hafifu ya kunyakua taji la kwanza kwenye Ligi Kuu England tangu 2003-04 baada ya wikiendi iliyopita kujikuta ikiachwa nyuma kwa pointi 11 na vinara Liverpool kufuatia kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa West Ham United. Usiku wa Jumatano, Arsenal ilimenyana na Nottingham Forest.

LONDON, ENGLAND: GWIJI wa Arsenal, Ian Wright amefichua wasiwasi wake juu ya mastaa watatu wa timu hiyo kwamba hawatasaini mikataba mipya - watabaki na iliyopo sasa hadi mwisho ili waondoke bure.

Arsenal imeweka matumaini hafifu ya kunyakua taji la kwanza kwenye Ligi Kuu England tangu 2003-04 baada ya wikiendi iliyopita kujikuta ikiachwa nyuma kwa pointi 11 na vinara Liverpool kufuatia kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa West Ham United. Usiku wa Jumatano, Arsenal ilimenyana na Nottingham Forest.

Matumaini ya Arsenal kushinda ubingwa msimu huu yamezidi kuyeyuka baada ya kocha Mikel Arteta kushindwa kusajili straika kwenye dirisha lililopita kitu kinachowagharimu kwa sasa kutokana na washambuliaji wote wa kikosi hicho kuwa majeruhi.

Uamuzi huo umewashtua mashabiki wengi wa Arenal, ikiwamo gwiji Wright, akihoji nini ulikuwa mpango wa timu kwenye dirisha la usajili. Na Wright anaamini kukosekana kwa mipango thabiti ya namna hiyo kwenye timu itawafanya wachezaji kama Gabriel Magalhaes, Bukayo Saka na William Saliba wasisaini mikataba mpya.

Wright alisema: “Unapozungumzia kusaini mikataba mipya kwa wachezaji kama Saka, Gabriel (Magalhaes), Saliba, kwa namna mambo yanavyokwenda kwa sasa, nabashiri ishu hiyo itakwenda taratibu sana.

“Tutakwenda kukabiliana na hali kama iliyotokea Liverpool kwa wachezaji Trent, Salah na Virgil.

“Hata mimi ningekuwa hao wachezaji, kisha klabu inasema ngoja tusubiri tuone wakati mimi mchezaji mkataba wangu uliopo ni wa miaka miwili, nitasubiri kuona ni mchezaji gani atasajiliwa dirisha kubwa.”

Wright, mtambo wa mabao wa zamani wa Arsenal anaamini Arteta anaweza kujikuta kwenye wakati huo mgumu wa wachezaji wake muhimu kushindwa kusaini mikataba mipya wakitaka uhakika wa ubora wa kikosi.