England yaanza kwa kishindo Qatar

DOHA, QATAR. ENGLAND imeanza kwa kishindo fainali za Kombe la Dunia Qatar kwa kuichapa Iran mabao 6-2 kwenye uwanja Khalifa International.
Mabao ya England yaliwekwa kimiani na Judde Bellingham dakika ya 35, Bukayo saka dakika ya 43 na 62, Raheem Sterling dakika 45, Marcus Rashford aliyeingia kipindi cha pili akitokea benchi akapachika bao dakika ya 71, msumari wa mwisho ukiwekwa nyavuni na Jack Grealish dakika ya 89.
Mabao mawili Iran ya kufutia machozi yalifungwa na Mehdi Tarem dakika ya 65 na 90, moja likiwa la mkwaju wa penalti, hata hivyo haikuwasaidia kuepuka kipigo hicho kwenye mchezo huu.
Mechi hiyo iliiongezwa jumla ya dakika za nyongeza 24 kufidia dakika zilizocheleweshwa baada ya kipa wa Iran, Alireza Beinranvand kuumia pua kipindi cha kwanza pamoja na Harry Maguire.