England inavyohaha kuingiza timu tano Mabingwa Ulaya

LONDON, ENGLAND. LIGI ya Mabingwa Ulaya inajiandaa kufanya mabadiliko ambayo yatashuhudia mataifa mawili makubwa kwenye viwango vya ubora wa Uefa kupata nafasi moja ya ziada kwenye ushiriki wa michuano hiyo kuanzia msimu ujao.

Kwa hali ilivyo sasa, Ligi Kuu England itapoteza nafasi moja ya ziada ili kuwa na timu tano.

Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa muda sasa imekuwa ikishirikisha timu 32 zilizogawanywa kwenye makundi manane yenye timu nne, ambapo timu mbili za juu zitavuka hatua inayofuata.

Lakini, msimu ujao mfumo utakuwa tofauti. Swali lililopo, je England itakuwa na timu ya ziada?

Vipi England itapata timu ya tano?

Timu zote sita za Ligi Kuu England zipo kwenye mikikimikiki kwa wiki mbili sasa ndani ya mwezi huu, ambapo Man City inaonekana kama imeshafuzu hatua inayofuata, huku pia mambo yakiwa mazuri kwa Liverpool, Brighton, West Ham na Aston Villa. Kama kama timu zote za Ligi Kuu England zitashinda, jumla ya pointi itakayokusanya kwenye viwango ni 2.75, ikiwamo bonasi na hapo, itafanya Ligi Kuu England kushika usukani kwenye msimamo wa viwango. Mbio hizo za kuwania nafasi ya tano kwenye ushiriki wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, itafahamika itakapofika Machi 14. Lakini, kwa kipindi hiki, ushindi wa Arsenal kwa FC Porto, utakuwa habari njema kwa Tottenham na Man United.

Mfumo mpya wa Ligi Mabingwa Ulaya ukoje?

Mfumo mpya utahusisha timu 36 ambazo zitawekwa kwenye msimamo mmoja, ambapo zitacheza kwa mtindo wa ligi, ambapo timu nane za juu kwenye msimamo, zitafuzu moja kwa moja kwenye raundi ya 16 bora, wakati timu namba 9 hadi 24 zitachuana kucheza mchujo kupata nane nyingine. Kupata ratiba ya nani acheze na nani, timu hizo zitawekwa kwenye mafungu manne yenye timu tisa. Kila timu itapangwa kukutana na timu mbili kutoka kwenye kila fungu ikiwamo fungu ambalo wao wamo. Hakuna timu itakayoangukia kwenye Europa League wakati mechi za makundi zitakapokamilika.

Kutokana na timu za Ligi ya Mabingwa Ulaya kuongezeka kutoka 32 hadi 36, hiyo ina maana kuna nafasi nne za kugombea. Nafasi mbili zitakwenda kwenye ligi ambayo klabu zake zimefanya vizuri kwenye michuano ya Ulaya, ikiwamo Europa League na Europa Conference League, msimu huu. Na nafasi mbili zitakwenda kwa timu inayoshika nafasi ya tatu kwenye timu zinazoshika nafasi ya tano kwenye viwango vya Uefa.

Viwango vya Uefa vinafanyaje kazi?

Ligi zinazofanya vizuri zitatazamwa kwa wastani kwa klabu zinazoshiriki kwenye michuano ya Ulaya. Kila ushindi kwenye klabu una thamani ya pointi mbili, sare pointi moja na kipigo hakina pointi yoyote. Pointi za ziada zinatolewa kwa ligi itakayovuka hatua mbalimbali kwenye michuano hiyo ya Ulaya. Kucheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya makundi, thamani yake ni pointi nne, pointi tano kwa hatua ya mtoano ya 16 bora na robo fainali, nusu fainali na fainali. Ushindi kwenye makundi ya Europa League, kama ambavyo Liverpool imefanya, thamani yake ni pointi nne, wakati pointi mbili kwa timu zitakazokuwa kwenye nafasi ya pili. Pointi za ziada hutolewa kwa timu iliyofika hatua ya 16 bora, robo fainali, nusu fainali na fainali. Kushinda mechi yako kwenye hatua ya makundi ya Europa Conference League, kama Aston Villa ilivyofanya, hiyo thamani yake ni pointi mbili, wakati kufuzu kama mshindi wa pili, thamani yake ni pointi moja. Pointi za ziada hutolewa kwa kwa kufika nusu au fainali.

Pointi zote zitakazokusanywa na kila nchi zitajumlishwa kisha zitagawiwa kwa idadi ya timu kutoka kwenye nchi husika iliyoshiriki michuano hiyo ya Ulaya, timu nane kwa kesi ya Ligi Kuu England.

Man United na Newcastle zimeshindwa kusonga mbele, hata kwenye Europa League, hivyo hilo limefanya Ligi Kuu England kushuka kwenye viwango vya Uefa hadi nafasi ya tatu.

Ligi Kuu Egland ilipata nafasi ya ziada kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu minne kati ya mitano iliyopita, ilikosekana kwenye msimu wa 2019-20. Kwa sasa kwenye viwango, Ligi Kuu England ina pointi 12.13, nyuma ya Ujerumani 13.36 na Italia 13.14. Kutokana na Man United na Newcastle kutupwa nje, Ligi Kuu England sasa inategemea timu zake zilizobaki kukusanya pointi ili kufika namba za juu kwenye viwango. Man City ilikuwa kinara kwenye kundi lake na Arsenal pia. Liverpool, Brighton na West Ham zote zimesonga mbele kwenye Europa League, wakati Aston Villa pia imefuzu hatua ya mtoano Europa Conference League. Kwa hali ilivyo hadi sasa, Bundesliga na Serie A zitapata nafasi za ziada kwenye ushiriki wao kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kama timu itakuwa kwenye nafasi za juu kwenye viwango vya Uefa kisha ikashinda ubingwa wa Europa League ikiwa haipo kwenye nafasi ya tano katika msimamo wa ligi ya ndani, basi nchi hiyo itakuwa na wawakilishi sita kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya kuanzia msimu ujao.

Arsenal yaombwa iokoe jahazi

Mashabiki wa Man United na Spurs bila ya shaka kwa usiku wa Jumatano walikuwa upande wa Arsenal wakiombea ishinde mchezo wake wa ugenini dhidi ya FC Porto huko Ureno.

Ligi Kuu England inahaha kupata nafasi ya ziada kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, ili iwe na washiriki watano, hivyo inahitaji timu zake zishinde ikiwamo Arsenal kukusanya pointi ambazo zitawasogeza hadi kwenye nafasi mbili za juu kwenye viwango vya ubora wa Uefa ili kupata nafasi hiyo ya ziada ya kuwa na timu tano katika michuano hiyo ya Ulaya kwa msimu ujao. Baada ya Man City kuichapa Copenhagen, Arsenal ilikuwa inasubiriwa iishinde Porto ili zipatikane pointi 0.5 za kuongezea pale kwenye pointi zao za viwango vya Uefa. Ushindi wa timu zote za Ligi Kuu England utawafanya kuvuna pointi 2.75 pamoja na bonasi, hivyo itasaidia England kupanda hadi nafasi ya kwanza kwenye viwango vya Uefa. Hapo, Ligi Kuu England itakuwa na uhakika wa kuwa na timu tano kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.