Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Emiliano Martinez anaitaka Man United

MARTINEZ Pict
MARTINEZ Pict

Muktasari:

  • Na kocha wa Mashetani Wekundu, Ruben Amorim anataka pia kufanya usajili wa kipa kwenye kikosi chake ili kuwa na mtu langoni kwa msimu ujao baada ya Andre Onana kudaiwa kuwa kwenye rada za Monaco.

BIRMINGHAM, ENGLAND: KIPA Emiliano Martinez amepanga kulazimisha dili la kwenda kujiunga na timu ya ndoto zake, Manchester United, imeelezwa.

Na kocha wa Mashetani Wekundu, Ruben Amorim anataka pia kufanya usajili wa kipa kwenye kikosi chake ili kuwa na mtu langoni kwa msimu ujao baada ya Andre Onana kudaiwa kuwa kwenye rada za Monaco.

Amorim anataka manahodha na viongozi kwenye kikosi chake huku bosi huyo wa Man United kwa muda mrefu akivutiwa na kipa huyo wa Aston Villa, 32, ambaye alichaguliwa kuwa Kipa Bora wa Mwaka wa Fifa mara mbili katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

Chanzo kilibainisha: “Emi ni rafiki mzuri wa mchezaji mwenzake wa Kiargentina Lisandro Martinez na yupo tayari kuhama. Na tayari amezigomea timu kadhaa kwa matumaini ya kujiunga na Man United.

“Amorim anamhusudu sana. Alijaribu kumsajili alipokuwa Sporting mwaka 2020, lakini alizidiwa na Aston Villa. Anataka kukijaza kikosi chake kwa kuwa na manahodha na viongozi na Emi ana vitu vyema kwenye hilo.”

Amorim tayari ameshamnasa Mbrazili na staa wa Wolves, Matheus Cunha kwa ada ya Pauni 62.5 milioni kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi akijaribu kujenga kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.

Lakin, kocha huyo Mreno sasa anaweza kumnasa staa mwingine wa Amerika Kusini, mshindi wa Kombe la Dunia 2022 alipokuwa na kikosi cha Arsenal, Martinez - ambaye atakwenda kuleta changamoto ya kugombea namba na kipa Onana na Altay Bayindir.

Onana amekuwa akihusishwa na mpango wa kuondoka Old Trafford baada ya kufanya makosa kibao kwenye timu hiyo tangu alipojiunga akitokea Inter Milan kwa ada ya Pauni 47 milioni, Julai 2023 na Monaco ya Ufaransa inafuatilia kwa karibu mpango wa kunasa huduma ya Mcamerooni huyo mwenye umri wa miaka 29.

Bayindir naye alishindwa kujibeba baada ya kuruhusu mabao anne katika mechi ya kipigo kutoka kwa Newcastle wakati alipopewa nafasi ya kumbadili Onana golini.

Martinez alisaini mkataba wa miaka mitano anaolipwa Pauni 150,000 kwa wiki huko Aston Villa kwa muda usiozidi mwaka, lakini klabu hiyo ya Villa Park imeshindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ofa yoyote inayoanzia Pauni 40 milioni inaweza kuwashawishi Aston Villa kumuuza kipa huyo.