Emilia na De Paul watikisa urafiki wa mastaa Argentina
Muktasari:
- Urafiki kati ya Emilia na Tini ulioonekana kuwa imara kati ya nyota hao wa muziki wa pop wa Argentina, lakini kwa sasa umeishia kuvunjika, na habari hiyo inazungumzwa sana nchini Argentina.
MIAMI, MAREKANI: UJUMBE wa simu ya mkononi unaodaiwa kutoka kwa Emilia Mernes kwenda kiungo nyota wa Inter Miami na Argentina, Rodrigo de Paul umevunja urafiki na Tini Stoessel, baada ya kuonekana wawili hao walikuwa wakitongozana.
Urafiki kati ya Emilia na Tini ulioonekana kuwa imara kati ya nyota hao wa muziki wa pop wa Argentina, lakini kwa sasa umeishia kuvunjika, na habari hiyo inazungumzwa sana nchini Argentina.
Uhusiano kati ya Tini na Emilia unaweza kuwa ulifikia mwisho baada ya mlolongo wa matukio yanayorejelewa ambapo tabia ya Emilia inasemekana kuibua taharuki miongoni mwa wake wa wachezaji wa soka maarufu nchini Argentina ambao hata hivyo wanacheza nje ya nchi yao. Tini ni mwandani wa De Paul. Kulingana na taarifa zilizovunja na kutolewa na kipindi cha Infama, usumbufu ulianza ndani ya sherehe za karibuni za timu ya taifa ya Argentina, ambapo mashuhuda wanasema wake wa wachezaji hawakuwa na mtazamo mzuri juu ya uwepo wa Emilia, ambaye alihudhuria akiwa na mpenzi wake, rapa Duki.
Katika kipindi hicho ilielezwa kuwa kundi la wake wa mastaa lilimuelezea msanii huyo kama mwizi wa waume wa watu na ana tabia ya kuchochea kuharibu uhusiano baina yao na waume zao, jambo ambalo limekuwa likisababisha mivutano katika familia zao.
Hata hivyo, kinachodaiwa kuwa siyo jambo linalofaa tu, bali uwepo wa mawasiliano ya moja kwa moja na ya faragha, inaelezwa kwamba msanii huyo amekuwa akituma ujumbe wenye taswira ya ngono kwa De Paul ambao hadi Tini ameshauona.
Nadharia hii inathibitishwa zaidi na ukweli kwamba, wakati wa tofauti ndogo ya awali kati ya Tini na kiungo huyo wa zamani wa Atletico Madrid anayecheza timu moja na Lionel Messi kwa sasa, alionekana akihudhuria tamasha la Emilia peke yake, ishara ambayo wakati huo haikuonekana kuwa na athari, lakini sasa inahusishwa na mapenzi. De Paul alitua Inter Miami Januari, mwaka huu akitokea Atletico Madrid katika uhamisho anaodaiwa kuulazimisha licha ya kwamba timu hiyo ya Hispania ilikuwa haitaki kumwachia.