Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Embolo aandika rekodi Switzerland

Muktasari:

  • Katika mechi hiyo ya kundi B ya Kombe la Dunia iliyopigwa kwenye Uwanja wa San Francisco Bay Area huko Santa Clara, California, Marekani imemfanya Embolo kuweka rekodi ya kufunga katika kila michuano minne iliyopita ya mashindano makubwa ya kimataifa.

BAO la dakika ya 17, lililofungwa kwa mkwaju wa penalti na mshambuliaji wa Switzerland, Breel Donald Embolo katika sare ya timu hiyo ya 1-1, dhidi ya Qatar, limefanya nyota huyo kuandika rekodi mpya kikosini humo, licha ya Boualem Khoukhi kuchomoa dakika ya 90+4.

Katika mechi hiyo ya kundi B ya Kombe la Dunia iliyopigwa kwenye Uwanja wa San Francisco Bay Area huko Santa Clara, California, Marekani imemfanya Embolo kuweka rekodi ya kufunga katika kila michuano minne iliyopita ya mashindano makubwa ya kimataifa.

Nyota huyo mzaliwa wa Cameroon anayecheza Klabu ya Rennes ya Ufaransa, alianza kuandika rekodi hiyo ya kufunga katika Michuano ya Euro mwaka 2020.

Katika Michuano ya Euro mwaka 2020, Embolo aliifungia bao Switzerland dhidi ya Wales kwenye hatua ya makundi na mechi hiyo kuisha sare ya kufungana 1-1, Juni 12, 2021.

Kwenye Michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika mwaka 2022, huko Qatar,  Embolo aliifungia Switzerland mabao mawili akianza na ushindi wa timu hiyo wa bao 1-0, dhidi ya Cameroon katika hatua ya makundi, Novemba 24, 2022.

Bao lingine la Embolo aliifungia Switzerland katika ushindi wa timu hiyo wa mabao 3-2, dhidi ya Serbia, ikiwa ni hatua pia ya makundi, mechi ikipigwa Desemba 2, 2022.

Kwenye Michuano ya Euro 2024, nyota huyo aliifungia Switzerland mabao mawili, akianza katika ushindi wa timu hiyo wa mabao 3-1, dhidi ya Hungary, ikiwa ni hatua ya makundi pia Juni 15, 2024.

Bao lingine kwa nyota huyo aliifungia Switzerland katika sare ya kufungana 1-1, dhidi England katika hatua ya robo fainali, kwenye mechi iliyopigwa Julai 6, 2024.

Kiwango hicho bora kwa nyota huyo amekiendeleza pia katika Michuano ya Kombe la Dunia 2026, baada ya kuifungia Switzerland bao katika sare ya timu hiyo ya 1-1, dhidi ya Qatar, Juni 13, 2026.

Bao hilo la nyota huyo limemfanya kuweka rekodi ya kufunga katika kila michuano minne iliyopita ya mashindano makubwa ya kimataifa.