Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Yaya Toure bado ana bifu na Guardiola

Muktasari:

  • Toure, 42, huko nyuma aliwahi kuzungumza kuhusu uhusiano wake mbaya dhidi ya Guardiola, kocha ambaye alimnoa Barcelona na Manchester City.

MANCHESTER, ENGLAND: KIUNGO, Yaya Toure ameamsha upya bifu lake na kocha Pep Guardiola na kumwita majina mabaya Mhispaniola huyo wakati alipofanyiwa mahojiano.

Toure, 42, huko nyuma aliwahi kuzungumza kuhusu uhusiano wake mbaya dhidi ya Guardiola, kocha ambaye alimnoa Barcelona na Manchester City.

Kiungo huyo Muivory Coast aliondoka Nou Camp kwenda kujiunga na Man City kwenye Ligi Kuu England mwaka 2010, baadaye alikuja kuungana tena na Guardiola wakati Mhispaniola huyo alipotua Etihad miaka sita baadaye.

Akishindwa kupata nafasi ya kuanza katika miaka yake miwili ya mwisho huko Man City, Toure aliibua jambo zito baada ya kudai Guardiola amekuwa na matatizo na wachezaji wa Kiafrika baada ya kuondoka kwenye timu hiyo, licha ya kwamba baadaye alidai alinukuliwa vibaya na kumwandikia ujumbe wa kumwomba radhi kocha huyo wa Man City.

Lakini, Toure ameibua jambo hilo upya akimshambulia Guardiola wakati alipokuwa akifanya mahojiano kwenye chaneli ya ZACK YouTube.

“Simwoni kama ni mtu, namwona kama nyoka tu,” alisema akikumbuka nyakati zake alizocheza chini ya Guardiola alipokuwa Hispania.

“Kocha wa Barcelona alinipigia kipindi kile na kuniambia 'unapaswa kurudi, ni muhimu.' Mke wangu aliniambia, 'hivi unamsikilia hayo mambo yake? Amekufanyia vibaya sana na sasa anataka ubaki? Hebu twende Manchester, kaka'ngu'.

“Yule jamaa hakuwa amenipanga kwa mwaka mzima na baada ya kwenda kung'ara kwenye Kombe la Dunia 2010. Mke wangu aliniambia kuhusu yule jamaa. 'Shetani, sio binadamu, ni mnyama.' Yeye anamwona kwamba sio mtu mwema kabisa.”

Tangu alipojiunga na Man City mwaka 2016, Guardiola ameshinda mataji sita ya Ligi Kuu England na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Toure akiwa chini ya Guardiola, walishinda pamoja mataji mawili ya kwanza ya Ligi Kuu England kabla ya kuondoka majira ya kiangazi 2018.