Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Duh! Morocco ilijiandaa mwaka na nusu

MOROCCO Pict

Muktasari:

  • Pazia la michuano ya AFCON 2025 limefunguliwa jana Jumapili Desemba 21, 2025 nchini Morocco ambapo kulikuwa na mechi moja kati ya wenyeji Morocco dhidi ya vijana kutoka visiwa vya Comoros iliyopigwa kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, jijini Rabat.

RABAT, MOROCCO: KOCHA wa timu ya taifa ya Morocco, Walid Regragui, amesema kikosi chake na benchi la ufundi kwa ujumla walijiandaa kwa mwaka mmoja na nusu kwa ajili ya kucheza mechi ya ufunguzi katika michuano ya AFCON 2025.

Pazia la michuano ya AFCON 2025 limefunguliwa jana Jumapili Desemba 21, 2025 nchini Morocco ambapo kulikuwa na mechi moja kati ya wenyeji Morocco dhidi ya vijana kutoka visiwa vya Comoros iliyopigwa kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, jijini Rabat.

Mechi hiyo ya Kundi A ilimalizika kwa Morocco kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ambayo yote yalipatikana katika kipindi cha pili dakika ya 55 kupitia kwa Brahim Diaz na dakika ya 74 lililofungwa na Ayoub El Kaabi.

Baada ya mechi hiyo, kocha Walid Regragui wa Morocco amesema: "Tulijiandaa kwa ajili ya hii mechi kwa takribani mwaka mmoja na nusu. Tulijipa presha sana wakati mechi inaanza na hatukucheza vizuri, tulikosa penalti na mwenzetu Romain Saiss akatolewa nje kwa majeraha. Tulipoenda mapumziko niliwaambia sikuwa nimeridhishwa na kile walichoonyesha, tulijadili namna ya kuboresha na haraka wachezaji walipokea maelekezo."

MOR 01

Kwa upande wake kocha wa Comoros, Stefano Cusin aliwasifia wachezaji wake kwa kiwango walichoonyesha katika mechi hiyo licha ya kupoteza.

"Tulikuwa tunajilinda vizuri sana, lakini kwenye mechi ya aina hii inapokuja nafasi moja unatakiwa kuitumia, sisi hatukufanya hiyo. Timu ilionyesha kiwango kizuri naamini hata wananchi wa Comoro watakuwa wanajivunia wao. Siwezi kusema tumecheza vibaya ndio maana tumepoteza mechi. Tulitengeneza nafasi ambazo hatukuzitumia. Mwisho Morocco ni timu nzuri tumekubali kwamba tumepoteza mbele ya timu bora," amesema.