Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Algeria yapata pigo kabla ya kuivaa Sudan

ALGERIA Pict

Muktasari:

  • Kwa upande mwingine, Abdelli hakuwepo kwenye orodha ya awali ya wachezaji 28 wa Algeria iliyotangazwa wiki iliyopita, jambo lililowashangaza wengi. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, aliyezaliwa Ufaransa, tayari ameichezea Algeria katika mechi nne za kimataifa.

KIUNGO nyota wa Algeria, Houssem Aouar, ameiondoa kikosi cha timu ya taifa kilichopo Morocco kwa ajili ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, ikiwa ni siku chache kabla ya kuvaana na Sudan mechi itakayopigwa keshokutwa jijini Rabat.

Kujiondoa kwa kiungo hiyo ni pigo kwa Algeria katika tumaini la kufanya vizuri huko Morocco ikiwa imepangwa Kundi E pamoja na nchi za Burkina Faso, Sudan na Guinea ya Ikweta.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka Algeria, Aouar alipata jeraha wakati wa mazoezi ya timu hiyo Alhamisi iliyopita, hivyo atalazimika kukosa michuano hioyo ya 35 inayopfanyikia Morocco.

Tayari benchi la ufundi la timu hiyo, imetangaza nafasi yake imechukuliwa Himad Abdelli wa klabu ya Angers ya Ufaransa. Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu aina ya jeraha hilo.

Abdelli hakuwepo kwenye orodha ya awali ya wachezaji 28 wa Algeria iliyotangazwa wiki iliyopita, jambo lililowashangaza wengi. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, aliyezaliwa Ufaransa, tayari ameichezea Algeria katika mechi nne za kimataifa.

Kwa upande wa Aouar, aliyewahi kuichezea timu ya taifa ya Ufaransa kabla ya kubadili na kuiwakilisha Algeria, alishiriki AFCON iliyopita iliyofanyika Ivory Coast miaka miwili iliyopita, ambako Algeria ilitolewa mapema kwa kushangaza.

Algeria itashuka uwanjani Jumatano kuvaana na Sudan kabla ya kukutana na Burkina Faso kisha kumalizana na Guinea ya Ikweta.

Kwa upande mwingine, Abdelli hakuwepo kwenye orodha ya awali ya wachezaji 28 wa Algeria iliyotangazwa wiki iliyopita, jambo lililowashangaza wengi. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, aliyezaliwa Ufaransa, tayari ameichezea Algeria katika mechi nne za kimataifa.