Duh! Kocha wa Lyon afungiwa miezi tisa

Muktasari:
- Fonseca, 52, alionekana kumbwatukia mwamuzi Benoit Millot mwinsoni mwa mchezo wa timu yake ya Lyon iliposhinda 2-1 dhidi ya Brest katika mchezo wa Ligue 1, Jumapili iliyopita.
PARIS, UFARANSA: KOCHA wa Olympique Lyon, Paulo Fonseca amefungiwa soka kwa miezi tisa baada ya kumvaa kimwili mwamuzi.
Fonseca, 52, alionekana kumbwatukia mwamuzi Benoit Millot mwinsoni mwa mchezo wa timu yake ya Lyon iliposhinda 2-1 dhidi ya Brest katika mchezo wa Ligue 1, Jumapili iliyopita.
Kocha huyo Mreno alikasirishwa na mwamuzi Millot baada ya kwenda kwenye skrini ya VAR kutazama tukio la penalti kwa Brest.
Kwenye tukio hilo, Fonseca alionekana kama anataka kumpiga kichwa Millot, akimbwatukia refa huyo usoni wakati alipokuwa akitoa kadi nyekundu kumwonyesha. Hakuna penalti iliyotolewa na Lyon iliondoka kwenye mechi hiyo na pointi zote tatu, ambayo ilikuwa ya tano kwa Fonseca tangu awe kocha wa kikosi hicho.
FLP ilithibitisha taarifa yake Jumatano iliyopita kwamba Fonseca amefungiwa na kwamba hatakaa kwenye benchi la ufundi hadi Novemba 30. Na kwenda mbali, Fonseca, 52, hataruhusiwa kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia vya mastaa wa Lyon kabla na baada ya mechi ya kishindani hadi Septemba 15.
Akizungumzia adhabu ya kufungiwa miezi tisa, Sebastien Deneux, rais wa kamati ya nidhamu, alisema: “Fonseca ni kocha wa Ligue 1. Ni mwelevu wa mambo mengi. Lakini, tabia zake zimekuwa tofauti kabisa. Kamati imemkuta Fonseca na hatia kumfanyia vitu vya hovyo mwamuzi, kumpigia kelele na pia kujaribu tukio la kumpiga kichwa kwa kuunganisha kichwa chake kwa refa huyo, ametimshia.”
Fonseca, amgaye alifutwa kazi AC Milan mapema msimu huu, aliomba radhi kwa tuko hilo, alisema. “Naomba radhi kwa kitendo chengu, sikupaswa kufanya vile.”
Adhabu ya Fonseca imekuja wiki moja baada ya rais wa Marseille, Pablo Longoria kufingiwa mechi 15 baada ya kudai kwamba waamuzi wa Ufaransa wanapokea rudha kufuatia timu yake kukutana na kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Auxerre. Huko kwenye Ligue 2, kocha wa Bastia, Benoit Tavenot alifungiwa mechi 12.