Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Drafti ijayo ya NBA ni vizazi vya wakongwe?

Muktasari:

  • Cameron na Cayden Boozer kila mmoja ana lengo la kufika NBA kama baba yao, Boozer aliyewahi kuwa mchezaji bora na staa katika kikosi cha All-Star mara mbili. Kwa sasa wote wawili wanatikisa katika mashindano ya vyuo wakiwa na lengo moja tu kuhakikisha kwamba mwakani wanapenya kwenye uchaguzi huo.

WINSCONCIN, MAREKANI: WATOTO wa staa wa zamani wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), Carlos Boozer wanakiwasha haswa katika mashindano ya vyuo huko Marekani, wakiisaka nafasi ya kuchanguliwa katika 'draft' ya mwakani ya kucheza katika michuano hiyo mikubwa duniani inayofuatiliwa zaidi.

Cameron na Cayden Boozer kila mmoja ana lengo la kufika NBA kama baba yao, Boozer aliyewahi kuwa mchezaji bora na staa katika kikosi cha All-Star mara mbili. Kwa sasa wote wawili wanatikisa katika mashindano ya vyuo wakiwa na lengo moja tu kuhakikisha kwamba mwakani wanapenya kwenye uchaguzi huo.

Draft ya NBA ni mchakato wa kila mwaka ambao timu zinazoshiriki ni zile zinazocheza mashindano hayo kuchagua wachezaji wapya kujiunga na ligi. Mara nyingi wachezaji wanaochaguliwa ni wale wanaocheza vyuo, sekondari (kwa kipindi maalumu kihistoria) na kutoka ligi nyingine kubwa nje ya Marekani.

Akiwa chuoni, Cameron anakipiga zaidi kwa sasa kwenye kiwango cha nyota tano na alikubali kujiunga na Duke Blue Devils badala ya Miami, Kentucky na Florida 2024, pamoja na ndugu yake pacha Cayden.

Mapacha hao walichagua kufuata nyayo za baba yao kujiunga na Brotherhood, kwani yeye alisoma Duke kati ya 1999–2002 na kushinda ubingwa wa taifa wa Shirikisho la Kikapu la Vyuo Marekani (NCCA) 2001.

Wote wawili, hususan Cameron, wanatarajia kuendelea kufuata nyayo za baba yao katika safari ya kuifuata NBA na kuwa mastaa wapya katika orodha inayopanuka ya baba na wana waliowahi kucheza ligi hiyo. Kwa sasa ni Lebron James pekee anayeichezea Los Angeles Lakers ndiye mwenye mtoto anayekipiga NBA, akicheza na mwanawe Ronny James katika kikosi hicho.

Baba yao Carlos alichaguliwa na Cleveland Cavaliers kama chaguo la 35 mwaka 2002, ambapo aliwahi kudai kwamba Cavaliers walikuwa na wachezaji bora kuliko mwamba wa baadaye NBA, LeBron James, ambaye wakati huo alikuwa bado hajachaguliwa. Carlos alicheza misimu 13 NBA akitwaa tuzo ya NBA All-Star mara mbili akiwa na Utah Jazz.

Mchezaji huyo anayekipiga kama power forward mwenye urefu wa futi 6 na inchi 9, pia aliitumikia Chicago Bulls kwa misimu minne kabla ya kujiunga na Los Angeles Lakers kwa msimu mmoja 2015, kisha akastaafu akiwa na umri wa miaka 33.

Alihitimisha maisha yake NBA akiwa amecheza mechi 861, akiwa na wastani wa pointi 16.2, wastani wa ribaundi 9.5 na asisti 2.2 na mitupo ya mbali asilimia 52.1. Baada ya kumaliza maisha yake ya uchezaji akihusisha pia kipindi kifupi nchini China alikokuwa akikipiga Guangdong Southern Tigers na kushiriki kwenye ligi ya BIG3, alirejea NBA kufanya shughuli nyingine nje ya uwanja.

Hata hivyo, asipokuwa bize kwa sasa husaidia uongozi wa timu wanayocheza wanawe kufanya uamuzi na huwafuatilia vilivyo wakicheza katika chuo chake.

Baada ya pacha hao kukubali kujiunga na Duke, baba yao alisema: “Najivunia sana. Wamefanya kazi kwa bidii kufikia wakati huu. Nimefurahishwa kwamba walichukua muda. Wameamua kucheza pamoja chuoni, jambo ambalo ni la ajabu. Wanaendana vizuri.

"Wamefanya uamuzi bora kwao. Mimi na mama yao hatungeweza kujivunia zaidi itakuwa safari ya kufurahisha.”


WANAWE HAWA HAPA

Kinachoelezwa na wachambuzi wengi wa kikapu kwa sasa ni kwamba, Cameron anaweza kuwa chaguo la juu la tatu katika NBA mwakani.

Cayden, mlinzi mwenye urefu wa futi 6 na inchi 5 amejitokeza ndani ya 20 bora za mtandao maarufu wa michezo wa ESPN akiwa nafasi ya 17, na anachukuliwa kuwa mchezaji wa tano kwa ubora katika nafasi anayocheza. Kwa wastani wa dakika 22.3 tangu kuanza kwa msimu, ana wastani wa pointi 7.4 kwa uchezaji wa asilimia 48.4 eneo analocheza pamoja na ribaundi 3.0, asisti 4.0 na uporaji wa mipira (steals) 1.1.

Cameron kwa upande wake ambaye ana inchi nne zaidi ya ndugu yake, ni power forward mwenye urefu wa futi 6 na inchi 9 kama baba yake, na ESPN ilimpanga nafasi ya pili katika mastaa 100 wanaokuja juu kwa kasi kwenye kikapu kwa sasa.

Wakati fulani, alikuwa anaorodheshwa mbele ya Cooper Flagg ambaye alikuwa chaguo namba moja katika drafti ya NBA mwaka huu na nyota wa zamani wa Duke. Flagg anaichezea Dallas Mavericks.

Msimu wa 2025–26 wa kikapu wa wanaume NCAA ukiwa umeanza hivi karibuni, Cameron hajapoteza muda kuonyesha kwamba yupo tayari kwani katika mechi saba za kwanza zote za ushindi, mshindi huyo mara mbili wa tuzo ya Gatorade Player of the Year anaongoza timu katika takwimu zote kubwa akiwa na wastani wa pointi 21.1 kusukuma mashambulizi, ribaundi 9.9, asisti 4.0, uporaji mipira 1.7 na kuzuia 1.3.

Katika makadirio ya karibuni ya ESPN, Cameron anatabiriwa kuchaguliwa nafasi ya tatu nyuma ya nyota wa Kansas Jayhawks na anayependekezwa kama chaguo namba moja Darryn Peterson na Anicet 'AJ' Dybantsa Jr.


MWINGINE HUYU HAPA

Mara ya mwisho Carmelo Anthony aliichezea Los Angeles Lakers kwa muda mfupi kuanzia 2021–2022 na baada ya hapo akawa ubaoni, hana timu. Staa huyo mkongwe aliishi bila timu kwa miezi 17 kwani ilipofika Mei 22, 2023 alistaafu na kushika hamsini zake kuendeleza biashara zake.

Lakini, huku nyuma kama ilivyo kwa LeBron ambaye ni mzazi wa Ronny, Carmelo ana mwanawe ambaye ni staa mpya wa kikapu na wakati wowote baada ya msimu ujao huenda akashuhudiwa akikipiga katika timu kubwa.

Kiyan Anthony, mtoto wa Carmelo, kwa sasa anakiwasha katika timu ya Chuo Kikuu cha Syracuse kwenye mashindano ya vyuo akijaribu kufuata nyayo za baba yake.

Kiyan akiwa na umri wa miaka 18 huenda ndiyo kwanza ameanza safari yake, lakini tayari ameanza kujitokeza kama nyota anayechipuka, na huenda akaibuka na kufuata nyayo za watoto wa mastaa wengi wa kikapu waliopita na waliopo akiwamo Ronny ambaye ni mtoto wa Lebron.

Miongoni mwa kundi dogo la nyota chipukizi vyuoni wenye matarajio ya kufuata nyayo za baba zao NBA, Kiyan anapambana kufanya hivyo. Licha ya kupata ofa kutoka timu kubwa za kikapu zinazocheza NCAA zikiwamo Auburn Florida State, Ohio State na USC, lakini ameamua kwanza aendelee kujitafuta akiwa timu ya kati.

Katika michezo minne ya kwanza hivi karibuni, fowadi huyo mwenye urefu wa futi 6 na inchi 5 ameibuka na wastani wa pointi 14.8 kila mchezo, ribaundi 3.0 na asisti 1.8 kwenye kila dakika 26.8 za mchezo.

Timu yake ya Syracuse imeuanza msimu kwa ushindi wa 4-0 ikiwazidi wapinzani wake kwa wastani wa pointi 29 kwa kila mchezo. Ripoti ya utafiti ya NBA inaonyesha dogo huyo anaweza kuwa mlinzi au fowadi bora mwenye uwezo wa kufungua uwanja na kutupa mipira ya mbali kwa ufanisi.


NJIA YA BABA

Baba wa Kiyan, Carmelo Anthony alitumia msimu wake wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Syracuse 2002–03, ambako aliiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa kwanza na pekee hadi sasa wa Marekani ambao iliuchukua.

Fowadi huyo mwenye urefu wa futi 6 na inchi 7 alikuwa sehemu ya drafti ya NBA 2003 ambapo alichaguliwa na Denver Nuggets kama chaguo la tatu nyuma ya mmoja wa wachezaji bora wa kikapu wa wakati wote - LeBron James na bingwa wa NBA wa 2004 akiwa na Detroit Pistons, Darko Milicic. Chris Bosh (Toronto Raptors) na Dwyane Wade (Miami Heat) walikamilisha drafti tano za juu za kile kinachokuwa mojawapo wa drafti bora kabisa za wakati wote.

Carmelo alitumia miaka saba na nusu ya kwanza NBA akiwa na Nuggets kabla ya uhamisho wa kushangaza katikati ya msimu kwenda New York Knicks ambako aling’ara. Baada ya uteuzi mara sita mfululizo katika kikosi cha All-Star akiwa New York Knicks alihamia Oklahoma City Thunder.

Kuanzia wakati huo alikuwa kama msafiri akipita kwa vipindi vifupi Houston Rockets, Portland Trail Blazers na Los Angeles Lakers kabla ya kustaafu 2023 akiwa na umri wa miaka 37 baada ya kudumu kwa miaka 19 katika ligi hiyo ya kikapu.