Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dorgu asifiwa kukataa penalti

DORGU Pict

Muktasari:

  • Man United ilitinga robo fainali ya Europa League baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wapinzani wao hao kutoka Hispania katika mchezo uliofanyika Alhamisi usiku.

MANCHESTER, ENGLAND: MASHABIKI wa soka wamemmwagia sifa kedekede Patrick Dorgu baada ya beki huyo wa Manchester United kufanya tukio lililoonekana kuwa la kiungwana katika mechi dhidi ya Real Sociedad.

Man United ilitinga robo fainali ya Europa League baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wapinzani wao hao kutoka Hispania katika mchezo uliofanyika Alhamisi usiku.

Kiungo Bruno Fernandes alifunga hat-trick uwanjani Old Trafford, huku mabao mawili akifunga kwa penalti. Diogo Dalot alifunga bao la nne, kuifanya Man United kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-2 na sasa itakwenda kumenyana na Lyon ya Ufaransa kwenye robo fainali.

Bao pekee la Sociedad kwenye mechi hiyo ya marudiano nalo lilifungwa kwa mkwaju wa penalti, jambo lililofanya usiku huo kushuhudiwa penalti tatu. Lakini, kulikuwa na penalti nne zilizotolewa kwenye Theatre of Dreams.

Dorgu alionekana kama vile ameangushwa ndani ya boksi na mchezaji Hamari Traore.

Wakati Fernandes akijiandaa kwenda kupiga penalti nyingine dhidi ya Sociedad iliyokuwa na wachezaji 10 uwanjani baada ya mwamuzi Benoit Bastien kuipa penalti ya tatu wa Man United, beki huyo wa kushoto, Dorgu alimfuata mwamuzi na kumwambia kwamba hakufanyiwa madhambi.

VAR kisha ilihusishwa, marudio ya video yalionekana Traore aligusa mpira kabla ya kumwaangusha Dorgu ndani ya boksi. Dorgu alisifiwa na kitendo cha kuonyesha kuwa ni mwanamichezo, ambapo mwamuzi Bastien alibadili uamuzi wake wa kuacha kuipa penalti Man United.

Jambo hilo liliwaibua mashabiki, ambapo mmoja alisema: "Ni aibu kuona vitu kama hivyo vimekuwa nadra kwenye soka, uanamichezo wa hali ya juu."

Mwingine alisema: "Mwanamichezo mahiri, safi kijana."

Shabiki mwingine alisema: "Walau kaka amekuwa muungwana."

Kuna shabiki alisema: "Uanamichezo wa hali ya juu kwenye mchezo ambao hauna matukio ya hivi ya kutosha, umefanya vizuri Dorgu."

Kocha wa Man United, Ruben Amorim, naye alivutiwa pia na kitendo hicho cha Dorgu, aliposema: "Kilikuwa kitu sahihi kufanya, najivunia sana, lakini nisingesema hivyo kama matokeo yangekuwa 0-0 au kwamba tunapoteza mechi, majibu yangu yasingekuwa haya."