Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Doku kuikosa Iran, kauli juu ya mtoto yatikisa

Muktasari:

  • Taarifa ya kutokuwepo kwa Doku imekuja siku chache baada ya nyota huyo wa Manchester City kuweka wazi kuwa yupo tayari kuondoka kambini iwapo itahitajika ili kuhudhuria kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza.

LOS ANGELES, MAREKANI: WAKATI Ubelgiji ikijiandaa na mechi ya pili ya kundi G ya  Kombe la Dunia, winga wa timu hiyo, Jeremy Doku ataukosa mchezo huo baada ya shirikisho la soka la nchi hiyo kutangaza kuwa anasumbuliwa na maradhi.

Hata hivyo, haikulezwa mchezaji huyo anasumbuliwa na maradhi gani.

Taarifa ya kutokuwepo kwa Doku imekuja siku chache baada ya nyota huyo wa Manchester City kuweka wazi kuwa yupo tayari kuondoka kambini iwapo itahitajika ili kuhudhuria kuzaliwa kwa mtoto wake wa kwanza.

Doku, mwenye umri wa miaka 24, alisema mkewe Shireen anatarajiwa kujifungua wiki ya pili ya Julai, kipindi ambacho kinaweza kuingiliana na hatua ya robo fainali ya Kombe la Dunia ikiwa Ubelgiji itafanikiwa kufika hatua hiyo.

"Ni mtoto wangu wa kwanza, hivyo bila shaka ningependa kuwepo wakati wa kuzaliwa kwake," alisema Doku.

Kauli hiyo ilizua mjadala huku mashabiki, wachambuzi na wanamichezo wa zamani wakigawanyika kuhusu jambo hilo.

Inaelezwa kwamba wapo walioamini kuwa hakuna jambo muhimu zaidi kwa mzazi kuliko kushuhudia kuzaliwa kwa mtoto, lakini wengine wanaamini Kombe la Dunia ni tukio la kipekee ambalo halipaswi kuwekwa pembeni kwa sababu yoyote.

Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha L'Equipe nchini Ufaransa, France Pierron alisema: "Huwezi kukosa Kombe la Dunia. Mtoto atakuwepo siku zote."

Kauli hiyo ilipingwa na bondia wa zamani wa Ufaransa, Brahim Asloum ambaye alisisitiza kuwa familia ni muhimu kuliko mashindano yoyote ya michezo.

"Mtoto ni maisha yako yote. Kombe la Dunia lina mwisho wake lakini familia inabaki milele," alisema Asloum.

Kutokana na ukosoaji mkubwa alioupata, Pierron baadaye alitoa ufafanuzi na kuomba radhi kwa wale waliohisi kauli zake zilidharau nafasi ya baba katika familia.

Wakati hayo yakiendelea, Doku bado hajafanya uamuzi wa mwisho kuhusu suala la kuondoka kambini.

Doku sio mchezaji wa kwanza kukumbana na hali hiyo. Katika miaka ya karibuni, nyota wa Ufaransa Kingsley Coman aliwahi kuondoka kambini wakati wa Euro 2021 na Euro 2024 ili kuhudhuria kuzaliwa kwa watoto wake.

Kiungo wa Liverpool, Ryan Gravenberch, pia aliwahi kukosa mchezo wa Ngao ya Jamii England baada ya kuwa baba, wakati nyota wa soka la Kimarekani, Shohei Ohtani wa Los Angeles Dodgers alipewa ruhusa maalumu kuhudhuria kuzaliwa kwa mtoto wake wa pili.