Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Diego Simeone anamtaka Rashford Atletico Madrid

FUNUNU Pict

Muktasari:

  • Rashford ameonekana kurejea  katika kiwango chake akiwa Camp Nou, jambo linaloendelea kuwavutia vigogo wengi barani Ulaya.

ATLETICO Madrid imeonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa England, Marcus Rashford, 28, ambaye kwa sasa anachezea Barcelona kwa mkopo akitokea Manchester United.

Rashford ameonekana kurejea  katika kiwango chake akiwa Camp Nou, jambo linaloendelea kuwavutia vigogo wengi barani Ulaya.

Inaelezwa kuwa Rashford hana mpango wa kurejea Manchester United hata kama Barcelona haitafanikiwa kumaliza mchakato wa kumsainisha mkataba wa moja kwa moja, hali inayotoa matumaini kwa Atletico Madrid kuingia rasmi kwenye dili hilo.

Barcelona ina kipengele cha kumnunua moja kwa moja nyota huyo mwishoni mwa msimu, lakini changamoto kubwa kwao ni gharama ya uhamisho pamoja na mshahara wake mkubwa, jambo linaloweza kuwafanya kushindwa kumudu usajili wake.

Kocha Diego Simeone anaamini Rashford anaweza kuendana vyema na mfumo wake wa ushambuliaji kutokana na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja.

Rashford, ambaye mkataba wake na Manchester United unamalizika   mwaka 2028, akiwa na Barca tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 23 za michuano yote, amefunga mabao saba na kutoa asisti 11.


Antoine Semenyo

MANCHESTER  United nayo imepanga kuingia mazima ili kumsajili mshambuliaji wa Bournemouth na timu ya tajfa ya Ghana katika dirisha lijalo la majira ya baridi.

Mashetani hao wekundu wanaamini kutoeleweka kwa hatma ya kocha Pep Guardiola wa Man City inaweza kuwa faida moja wapo ya wao kumpata Semenyo kwani majirahi zao hao wanaonekana kuwa tishio katika vita hiyo mbali ya Liverpool.

Semenyo mwenye umri wa miaka 25, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwa 2030.

Msimu huu amecheza mechi 16 za michuano yote na kufunga mabao saba.


Ruben Neves

STAA wa kimataifa wa Ureno,  Ruben Neves mwenye umri wa miaka 28, amekataa ofa ya mkataba mpya wa kuendelea kusalia katika kikosi cha Al-Hilal  ya  Saudi Arabia na badala yake anataka kurejea barani Ulaya ambako timu kibao zinahitaji huduma yake ikiwa pamoja na Manchester United.

Staa huyu wa zamani wa Wolves aliamua kutimkia Saudi hapo awali kutokana na kiasi kikubwa cha pesa alichowekewa mezani kama mshshara.

Mkataba wake wa sasa na Al-Hilal unatarajiwa kumalizika mwisho wa msimu huu.


Kobbie Mainoo

MANCHESTER United imesisitiza haitamuachia kiungo wao Kobbie Mainoo, 20, katika dirisha la usajili la Januari isipokuwa kama itapokea ofa kubwa sana ambayo itakuwa ngumu wao kuikataa.

Inaelezwa kuwa Man United pia hawako tayari kumtoa Mainoo kwa mkopo, wakiamini bado ni sehemu muhimu ya mipango yao ya muda mrefu licha ya ushindani mkubwa wa namba katika safu ya kiungo unaosababisha asipate nafasi kubwa ya kucheza.

Mkataba wa sasa wa Mainoo unatarajiwa kumalizika mwaka 2027 na una kipengele kinachoiwezesha Man United kuurefusha kwa mwaka mmoja zaidi.


Djylian N’Guessan

SAINT-ETIENNE imekataa ofa ya awali ya Euro 8 kutoka Chelsea kwa ajili ya mshambuliaji wao chipukizi Djylian N’Guessan mwenye umri wa miaka 17.

Hata hivyo, klabu hiyo ya Ufaransa ipo tayari kuisikiliza Chelsea ikiwa itarudi mezani na ofa ya Euro 12.5  milioni 12.5, kiasi ambacho Etienne inaamini kinaendana na kipaji cha mchezaji huyo.

N’Guessan anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji bora  vijana kutoka Ufaransa na mbali ya Chelsea kuna kundi kubwa la timu ambazo zinahitaji saini yake.


Bruno Fernandes

IMEFICHUKA kuwa kiungo na kapteni wa Manchester United, Bruno Fernandes, 31, ana kipengele maalum kwenye mkataba wake kinachoruhusu klabu zilizo nje ya Ligi Kuu England kumsajili kwa dau la Pauni 56.6 milioni.

Kipengele hicho kinaifanya Man United kuwa katika hatari ya kumpoteza nyota wao endapo klabu kubwa kutoka Ulaya au Mashariki ya Kati itaamua kulipa kiasi hicho na Bruno mwenyewe akawa tayari kuondoka.

Fernandes amekuwa mchezaji muhimu Old Trafford tangu ajiunge na klabu hiyo.


Nicolas Jackson

BAYERN Munich inaelezwa kuwa haina mpango wa kutumia kipengele cha kumsajili moja kwa moja mshambuliaji wa Chelsea, Nicolas Jackson, 24, mwishoni mwa msimu.

Jackson, raia wa Senegal, amekuwa akitumika zaidi kama mchezaji wa akiba mbele ya staa Harry Kane, 32, hali iliyopunguza nafasi yake ya kubakia mazima katika kikosi hicho.

Hata hivyo, ripoti zinadai Jackson hana mpango wa kurejea Chelsea hata kama Bayern isipomsainisha mkataba wa moja kwa moja.


Bukayo Saka

ARSENAL ipo hatua za mwisho kumsainisha mkataba mpya wa kihistoria nyota wao wa kimataifa wa England, Bukayo Saka, 24, utakaomuweka katika kikosi hicho  hadi mwaka 2031.

Kupitia mkataba huo, Saka anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Arsenal kulipwa mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki.

Uongozi wa Arsenal unaamini kumbakisha Saka ni hatua muhimu katika kulinda msingi walioujenga katika kikosi chao ambao kwa sasa matunda yake yameanza kuonekana.