Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Didier Drogba amtetea Mourinho Uturuki

Muktasari:

  • Mourinho, ambaye kwa sasa ni Kocha wa Fenerbahce, amejikuta kwenye hatari ya kufunguliwa mashtaka na wapinzani wao Galatasaray ana mambo ya kibaguzi.

ISTANBUL, UTURUKI: GWIJI wa Chelsea, Didier Drogba amemtetea kocha Jose Mourinho kutokana na tuhuma za ubaguzi, huku akimwelezea Mreno huyo ni “baba” yake.

Mourinho, ambaye kwa sasa ni Kocha wa Fenerbahce, amejikuta kwenye hatari ya kufunguliwa mashtaka na wapinzani wao Galatasaray ana mambo ya kibaguzi.

Gala ilitangaza mpango huo wa kumfungulia mashtaka Mourinho akidai amekuwa na mambo ya kibaguzi kwa watu wa Uturuki. Hilo limetokana na kauli ya Mourinho aliyotua wakati timu hizo zilipokutana hivi karibuni katika mechi ya suluhu. Fenerbahce imesimama na kocha wao, wakisema maneno hayo hayana maana yoyote.

Baada ya kucheza chini ya Mourinho huko Chelsea, Drogba alitumikia mwaka mmoja na nusu Galatasaray na kushinda ubingwa wa Super Lig mwaka 2013. Straika huyo wa zamani wa Ivory Coast ameibuka kumtetea bosi wake wa zamani, ambaye walikuwa na uhusiano mzuri sana walipokuwa pamoja Old Trafford.

“Wapendwa @GalatasaraySK, mnafahamu jinsi ninavyojivunia kuwahi kuvaa jezi za njano na nyekundu na mapenzi niliyonayo kwa klabu ya mataji Uturuki!!” aliandika Drogba kwenye mtandao wa kijamii.

“Sote tunafahamu upinzani uliopo na nimekuwa mwenye bahati kupata uzoefu wa jambo hilo. Nimeona madai ya kuhusu Jose Mourinho. Amini ninachowaambia, namfahamu Jose kwa miaka mingi, si mbaguzi na hana historia hiyo iwe zamani au sasa, naweza kuthibitisha hilo.

“Tuwekeze akili yetu kwenye mechi zetu, Tupambane tushinde ubingwa tupe zile nyota tano,” aliongeza kwa kusema nyota nne zilizopo kila mmoja inaelezea mataji matano ya ligi na kusema. “Hivi ‘baba’  yangu anakuwaje mbaguzi. Amkeni wandugu.”

Mourinho alichukua mikoba ya kuinoa Fenerbahce, Juni 2024, miezi mitano baada ya kuachana na AS Roma. Klabu hiyo ya Istanbul inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo, pointi sita nyuma ya Gala, lakini ipo pointi 12 juu ya timu inayoshika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo.