Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dharau zamponza Garnacho, awekwa benchi dhidi ya Atalanta

Muktasari:

  • Garnacho, 21, aliwakera mashabiki wa Italia kwenye mkutano huo wa Jumatatu wakati aliposema hajawahi kuitazama Atalanta ikicheza kwa zaidi ya mwaka mmoja.

LONDON, ENGLAND: ALEJANDRO Garnacho ameishia kuwekwa benchini kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Chelsea na Atalanta kutokana na kile alichokizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari.

Garnacho, 21, aliwakera mashabiki wa Italia kwenye mkutano huo wa Jumatatu wakati aliposema hajawahi kuitazama Atalanta ikicheza kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Alisema: “Mara ya mwisho kuitazama Atalanta ilikuwa miaka miwili iliyopita kwenye fainali ya Europa League na walishinda.”

Vyombo vya habari vya Italia vimemshutumu mchezaji huyo kwa kuonyesha dharau hiyo, huku mashabiki nao wakimjia juu. Hivyo, mashabiki hao walifurahi kumwona Garnacho akianzia benchini katika mechi ya Chelsea uwanjani New Balance Arena.

Joao Pedro aliifungia bao la kuongoza Chelsea kwenye dakika ya 25 ya mchezo, lakini straika wa zamani wa West Ham United, Gianluca Scamacca alisawazishia Atalanta muda mfupi baada ya mapumziko.

Na winga Charles De Ketelaere alibadilisha hali ya mchezo dakika 10 kabla ya mechi kumalizika alipofunga bao la pili na kuipa Atalanta ushindi wa 2-1.

Kwenye hatua nyingine, Garnacho alisisitiza kwamba hajutii uamuzi wa kuondoka Manchester United kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi, akisema amepiga hatua kubwa kwa kuhamia Chelsea.

Alisema: “Wakati mwingine kwenye maisha unahitaji kubadili vitu ili kupiga hatua ya juu kama mchezaji. Nadhani ilikuwa wakati sahihi na klabu sahihi, hivyo ulikuwa uamuzi sahihi. Nilikuja hapa kucheza mpira wangu na kuonyesha ni mchezaji wa aina gani. Kitu muhimu ni kujiamini. Maresca amekuwa akizungumza na mimi kila wiki na nadhani nitakuwa bora.”

Winga huyo wa Kiargentina amefunga mara mbili tu katika mechi 14 alizochezea Chelsea tangu alipojiunga akitokea Man United, Agosti mwaka huu.