Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dembele awasambaratisha Majogoo Anfield

MATOKEO Pict

OUSMANE Dembele amefunga mabao mawili wakati Paris Saint-Germain ikiichapa Liverpool 2-0 na kufuzu hatua ya nusu fainali ya UEFA Champions League, ambapo sasa itakutana na mshindi kati ya Bayern Munich au Real Madrid.

PSG iliingia kwenye mechi ya marudiano usiku wa Aprili 14, 2026 ikiwa na faida ya mabao 2-0 iliyopata nyumbani wiki iliyopita, lakini ililazimika kupambana sana kwenye Dimba la Anfield lenye shamrashamra, hadi pale Dembele alipofunga bao dakika ya 72 kwa shuti zuri la mguu wa kushoto. Dakika za nyongeza baada ya kufika 90, mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or 2025 aliongeza bao la pili.

Ikichochewa na mashabiki wake, Liverpool maarufu Majogoo wa Anfield, ilijaribu kwa nguvu kutafuta kurejea kwa kishindo kama ilivyozoea barani Ulaya, lakini kikosi hicho cha Arne Slot kilishindwa kufunga dhidi ya mabingwa hao watetezi, na kwa msimu wa pili mfululizo wameondolewa na PSG.

MATO 01

Baada ya kiwango duni Paris wiki iliyopita ilipopoteza 2-0, Liverpool ilionekana bora zaidi Anfield dhidi ya timu hiyo ya Ufaransa na iliwapa upinzani mkubwa, lakini haikutosha.

Slot alimpa nafasi ya kuanza Alexander Isak kwa mara ya kwanza tangu Desemba 2025 na kumweka benchi Mohamed Salah, lakini Salah aliingia dakika ya 30 baada ya Hugo Ekitike kuumia na kutolewa nje.

PSG ndio iliyokuwa hatari zaidi kipindi cha kwanza, huku kipa wa Liverpool, Giorgi Mamardashvili akiokoa mipira ya Khvicha Kvaratskhelia na Dembele.

MATO 02

Dembele alikosa nafasi ya wazi alipopiga mpira juu ya lango akiwa amebaki na kipa pekee. Kwa upande mwingine, Marquinhos alifanya uokoaji mzuri kuzuia Liverpool kufunga.

Slot alifanya mabadiliko mawili mapumziko, akimtoa Isak na kumuingiza Cody Gakpo pamoja na Jeremie Frimpong kutoka na nafasi yake kuchukuliwa na Joe Gomez, na Liverpool ilianza kipindi cha pili kwa kasi lakini haikuweza kufunga.

Dakika ya 65 Liverpool ilipata penalti baada ya Alexis Mac Allister kuangushwa na Willian Pacho, lakini baada ya VAR kuingilia, mwamuzi Maurizio Mariani alibatilisha uamuzi huo.

MATO 03

Dakika saba baadaye, Kvaratskhelia alimpa pasi Dembele ambaye alimpita Mamardashvili kwa kasi na nguvu kutoka umbali wa yadi 20 na kufifisha matumaini ya Liverpool.

Wakati mashabiki wakianza kuondoka Anfield, Dembele alifunga tena kwa karibu baada ya kupewa pasi na Bradley Barcola.

Kichapo hicho cha jumla ya mabao 4-0 kinaifanya Liverpool kumaliza msimu bila taji lolote, huku ikiwa bado haijulikani kama itafanikiwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.