Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

De Zerbi hajakata tamaa, asisitiza kubaki EPL

SPURS Pict

Muktasari:

  • Tottenham ilionekana kuwa karibu kupata ushindi wao wa kwanza wa EPL tangu kuanza kwa mwaka 2026 baada ya bao la kuvutia la Xavi Simons kuwapa uongozi mwishoni mwa mchezo dhidi ya Brighton jana.

BRIGHTON, ENGLAND: KOCHA wa Tottenham, Roberto De Zerbi amesisitiza timu yake inaweza kushinda mechi zote tano zilizobaki Ligi Kuu England na kujinasua kutoka eneo la kushuka daraja.

Tottenham ilionekana kuwa karibu kupata ushindi wao wa kwanza wa EPL tangu kuanza kwa mwaka 2026 baada ya bao la kuvutia la Xavi Simons kuwapa uongozi mwishoni mwa mchezo dhidi ya Brighton jana.

Hata hivyo, Georginio Rutter alisawazisha  dakika ya 95 na kufanya ubao usome mabao 2-2.

Matokeo hayo yaliifanya Spurs kuendelea kusalia eneo la kushuka daraja, pointi moja nyuma ya West Ham United huku ikiwa imecheza mechi moja zaidi.

De Zerbi amesema: “Bado haijaisha. Tunajua hali ni ngumu, lakini bado kuna mechi tano, pointi 15 na timu hii ina uwezo wa kushinda mechi tano mfululizo. Sasa inaweza kuwa vigumu kuelewa ninachosema, lakini angalia kiwango cha wachezaji wetu, tunaweza kushinda zote.”

"Sijivuni, hasa katika kipindi hiki, lakini tuna ubora wa kupambana na kushinda mechi mfululizo. Wachezaji hawapaswi kufikiria sana, wanapaswa kunifuata na kunisikiliza. Najivunia kiwango chao. Wanacheza kwa moyo. Nasikitika tu kwa matokeo tunayopata nawaonea huruma mashabiki wetu."

Spurs inatarajiwa kusafiri kwenda kucheza dhidi ya Wolves Jumamosi ya wiki hii, De Zerbi amewataka wachezaji wake kurejea mazoezini Jumatatu wakiwa na tabasamu.

"Sina muda wa kuona wachezaji wangu wakiwa na huzuni. Tunapaswa kuwa chanya. Sipendi watu wanaolalamika au kufikiria vibaya. Wanapaswa kuwa imara na kujikita kwenye mechi dhidi ya Wolves na kuja mazoezini wakiwa na tabasamu, vinginevyo waende nyumbani.”

Pia alimsifu Simons na kuahidi kuwa ataendelea kung’ara zaidi, huku akikataa kumlaumu Danso kwa kosa la dakika za mwisho lililosababisha timu ipoteze.